Friday 24 May 2013

Mchezo wa pool

Pool
Jee wewe ni mpenzi wa mchezo huu wa pool mimi ni mpenzi sana wa Pool hivi unasemaje kuhusiana na vijana hawa walio buni meza ya pool ya udongo vijana hawa wata weza kutimiza ndoto yao ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mchezo huu

leo nipo kijijini ambapo niliwakuta wamejitengenezea neza ya udongo wa mfinyazi ulio bebwa na fito nyembamba na iliyo wokewa mashimo sita (6) .....mchezo hii wa hapa kijijini unatumia mti mrefu ambao ni fimbo ya kuchezea na mipira inayotumiwa ni ya matunda yajulikanayo kwa jina la Tura kwakweli ukiwaona wakicheza ni burudani tupu

ombi lao kwa wadau kuomba wabau kuingiza vifaa vya mchezo huu nchini kwa wingi ili hata vijana wa kijijini waweze kufaidika kama wenzao wa mjini

dai la kuwa mchezo huu una wapotosha watoto na vijana wengi na kushindwa kuzingatia masuala ya masomo yao walidai si kweli na kuongeza yakuwa mtoto au kijana atapotoka kimaadili kwa kupenda wao wenyewe tutashukuru kama maombi na mawazo yetu yatatiliwa maanani....

No comments:

Post a Comment