Sunday 28 April 2013

BENDERA YETU NA MAANA ZAKE

 MAPOLI YA KIJANI:
Tanzania kuna mapoli makubwa na yaliyo wakilishwa na sura ya Bendera yake ya Taifa rangi ya kijani





RANGI YA NJANO:
Inawakirisha Madini yaliyo sheheni ya ndani ya nchi yetu na yanayo wafanya Watanzania kujivunia na kutembea kifua mbele huu ni mtambo unao wakilisha uwepo wa madini na rangi yake ya njano

RANGI YA BLUU:
inawakilisha Mito , Maziwa, Bahari ...yaliyo sheheni samaki wengi na viumbe wengi waliyo ndani ya zawadi hii tiliyo pewa na Mungu wetu Tuulinde utajiri huu.

RANGI NYEUSI:
Inawakilisha watu wake walio kabidhiwa mamlaka hii wa kujivunia kwani bara la Afrika ni mali ya Waafrika ....tuvienzi vitu hivi..zawadi kubwa yuliyo pewa na MOLA

TEMBO WEUSI KATIKA POLI LA KIMISI


TEMBO WA TANZANIA  
Nchi yetu ya Tanzania tume bahatika sana nau ya ma kujaliwa kwa kutunukiwa na mola wetu kwa kupewa dhahabu ya macho yetu kwa kupewa utajiri usio weza kufutika katika mapaji ya macho yetu endapo sisi wa Tanzania tuta ulinda huu si mwingine bali ni mali asili zetu za nchi hii nazo ni pamoja na mapoli makubwa, Wanyama, Mito mikubwa, Mapango ya kale kama vile Amboni, maziwa, Bahari, Mpori yenye kuvutia...haya yote ni mambo ambayo yanatia nakshi sura ya nchi yeti ya Tanzania....

TEMBO WEUSI:
wanyama hawa wakubwa wanyonyeshao weamekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka nje ya nchi lakini kwa masikitiko makubwa wanekuwa wakiwindwa kwa kasi sana na kuangamizwa uhai wao na majangiri au watu wenye tamaa kwa ajili ya tamaa ya kujipatia PEMBE ZA TEMBO HUYU...kwa hiyo uangamizwaji mkuu umekuwa ukifanyika kwa nia ya kujipatia Utajili ....EEE MUNGU WANISURU TEMBO WETU WEUSI......

Thursday 25 April 2013

MPIRA WA KIKAPU

  
    


    




Mpira wa kikapi Tanzania ....unapo sema mpira wa kikapu basi wanao ufahamu watakwenda moja kwa moja katika timu za TAN-BLACKS, PAZI AU MORAN FREMZI, JESHI STAR'S, NGE..YA TANGA, BIMA, BEEEZ, JKT..TANESKO, TABORA, NK. lakini bila ya kutosahau timu za masekondari premaly, za mavyuo...

Timuzote hizi zimekuwa zikitoa ushindani mkubwa katika kuucheza mchezo huu wa mpira wa kikapo Tanzania kwani kulikuwepo na mashindano mengi kama vile Mashindano ya kimkoa, mashindano ya Taifa , mashindano ya Marehemu Nshiku, na kadharuka  kwani wachezaji wote walikuwa wakiucheza mchezo huu kama ndugu kitu kilicho pelekea wachezaji wake wote kuishi kwa kutambuana na kuelewana, kusaminiana katika shida na raha.....lakini si hilo tuu, UMOJA, USHIKAMANO, UZARENDO uliota mizizi na kati ya timu kwa timu, mchezaji kwa mchezaji, na hata familia moja ya mwanamichezo na nyingine....

 NATOA HESHIMA ZANGU KWA WACHEZAJI WENZANGU WA KATI YA MIAKA YA ...1970.....hadi nilipo acha kuucheza mpira huu na kubaki kuwa mshauri kwa vijana walio jitokeza na kushikilia hatami  *Hassan Kange, *Zonga *Abass mansuri* Raimond ndanshau* Mwalimu ddoto* Raphael Kibwando* Peter Mgonda* Andrew Kizenga Shundi* Mzee Malay* Natty Mdeme* Bruno Mdeme *Frolida* Frola Lee, * Eke Mwaipopo *Bruno *, Sesi Manyerere, * na wengine ambao sukuwataja ni kwamba tuna wakumbuka na tunawapa heshima katika mchezo huu wa mpira wa kikapu....

Picha hii tumeitumia kwa niaba ya Timu zote za mpira wa kikapu na wale walio jitoa kuupemnda npira/ mchezo huu tuna wapa AHSANT...

Wednesday 24 April 2013

UJENZI WA MNADA WA NG'OMBE KAKUNYU

Mnada wa kakunyu



 Pongezi za miminika kwa wananchi wa Kakunyu wasifiwa kuhusiana na nguvukali iliyofanyika katika ujenzi wa jengo la kuuziaji mifugo la kisasa lililojengwa kwa nguvu za wananchi wa Katahiyo huu ni sehemi ya jengo hilo






kiujumla wananchi wa Katahiyo wamejipongeza kutokana na ushirikiano wao mkuu katika eneo hilo kuwa ni wa ukombozi kwa wanakijiji hiki
Mnada  Mpya ..Kakunyu



Makaribisho kwa wafugaji katika eneo hili la lyabatura na Kakunyu kwa ujumla



Viongozi wajijadiriana

usafiri wa kwetu...hapa kijijini.

usafiri wa kwetu


swala la usafiri huku kwetu limekuwa na utata kwani mazao yatokanayo na mgomba yamekuwa yakitupa adha kubwa katika kuyasafirisha hivi kutakuwepo na njia gani nyepesi ya kusafirisha mazao yetu na kuyafikisha sokoni wakati masoko yetu yapo mbali na tuzitoapo ndizi zetu ukitaka kujua ukweli wa swala hili nitakukaribisha tuungane katika usafiri wetu huu wa kijijini kwetu ....
Jia panda ya Bugango...Kakunyu
Hii ni njia panda ya kwenda Ryabatura na Bugango mpakani mwa Tanzania na Uganda kunapo patikana mazao ya Migonga, Ulezi, Karanga, Mahindi Mihogo, nk...sasa wameongezewa mazao mengine ya biashara kama alizeti, Mtama, Kahawa, mpunga...




MKUU WA WILAYA MISSENYI ...ASEMA



VIONGOZI WA WILAYA YA MISSENYI
WAMWAGA NEEMA KATA YA KAKUNYU

 
Mkuu wa wilaya ya Missenyi

 
         Katika hali ya kutia moyo na yaneema yadhihirika katika Tarafa ya Kakunyu baada ya viongovi wa wilaya ya Missenyi kutinga katika vijiji hivyo na kujadili kwa kina jinsi ya kuboresha hali ya kilimo ndana ya maeneo pichani ni mkuu wa wilaya Mweshimiwa Nshiku, mwenye nguo ya bluu Kiongozi wa Tarafa ya Kakunyu, mwenye kofia mwenyekiti wa kijiji cha Bugango

NEMA:- Tayari maafisa kulimo na Mifugo wamiminika na kuanza kazi huku  Wakiweka mikakati ya kuinua kilimo Tarafani Kakunyu,

Neema ya mazao ya Mpunga, Alizeti, Kahawa, na masuala ya kilimo cha kitaalamu cha miminika Tarafani humu .
WANANCHI:-wananchi  tarafani hapa wapongeza juhudi zilizo fanywa na uongozi wa missenyi wa kukiboreshea kilimo Tarafani hapa,

MAAFISA UGANI:- Maafisa kilimo hawa wamefurahia sana kwa upokewaji wao Tarafani humu na kuahidi kutoa utaalamu wao kwa kasi zaidi na kubadilisha hali ya kilimo cha kizamani hadi kuwa cha kitaalamu

MAPAMBANO :- Maafisa kilimo waapa kupambana na magonjwa ya mazao kwa mfano wa gonjwa hili la MNYAUKO linali shambulia zao la migomba- wilayani Missenyi watoa

USHAURI:- Uongozi watoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu wote walio letwa Tarafani humu ili mafanikio yaweze kuwafikia kwa kasi yenye mafanikio…..




Sunday 21 April 2013

Bicon No.30 kijijini kwetu Kirashwa.

Bicon no.30 mpakani mwa Tanzania na Uganda.


ni majuzi tuu nilipokuwa kwenye ziara yangu maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Uganda niliona kunakitu ambacho kilicho nifurahisha mimi kukiona kwa macho na si ajabu pia na wewe unge pendezewa aidha kukiona au kukitembelea na kujifinza mengi kuhusiana na hili ni Biconi hii No 30 au 31 mpakani mwa Tanzania na Nchi ya Uganda ....

Mimi nilifika nikakusogelea kichuguu huki chenye kuvutia kilicho tengenezwa kwa mawe mengi yaliyo kuwa na muonekano wa kulima kidoge kulicho egemea mpaka na chenye kuonyesha uimara wenye ushujaa ndani na nje ya mipaka huu wa Tanzania na Uganda......

kama tnakumbuka katika zile enzi za Beli Cimfrens wali tenga mipaka kwahiyo huu ndio uridhi wetu wa Mpaka au Mkuza ...ukiwa unatoa sura ya kitalii huku kwetu maeneo ya kijiji cha  KILASHWA....kijiji kilichopo karibu na Bicon hii...

ZIJUE BAADHI YA PASSPOT ZA TANZANIA


Napenda kukuonyesha hati za kusafiria na kupata kuzitanbua kwakuwa hati hizi ni haki za kila Mtanzania mamlaka yenye haki ya kuzi toa hati hizi ni Idara ya Uhamiaji na kila moja ina mhisu mtu gani anaepaswa kuitumia .......

Passpoti ya Kijani..Passport:- hii hutumika na mtu yeyote ambae ni Raia wa Tanzania mwenye sifa ya kupewa hati hii ya matembezi..na kusafiria dunia nzima,

Passporti hii ya kwanza ya Bluu:- hii hitumika kwa nchi za Afrika Mashariki na husafiria kwa nchi hizo za Afrika mashariki,

Passport hii ya Pili ya Bluu:- ya service au Passpori ya wafanyakazi hitumiwa na wafanyakazi wa ngazi furari za juu ili kuweza kusafiri safari za kikazi..duniani,

Ya mwisho Diplomatic Passport:- passpoti hii ni maalum kwa viongozi wa serekali na ni ya upendeleo kwa watu maalimu kwa mfano wabunge, mawazili mabarozi nk..
NIVYEMA KUZITAMBUA HATI HIZI:



Viongozi walioongoza idara ya Uhamiaji -1961 ...2013

 Hama tunavyo jionea ramani yetu ta Tanzania na viongozi wake walio hudimia idara ya Uhamiaji Tanzania ni kama wafuatao:-kuanzia mwaka 1969 hadi 1993

(1)....Mh.Raphael Kubaga... mwaka 1969 hadi 1983
Afisa Uhamiaji Mkuu,

(2)....Mh.Mbwana Mohamedi Bakari ...mwaka 1983 hadi 1989
Mkurugenzi wa Uhamiaji

(3)....Mh.Ali A Mnyika.... mwaka 1989 hadi 1993
                                                   Mkurugenzi wa Uhamiaji
hawa ni viongozi wa kwanza katika idara ya Uhamiaji na ndiyo walio ichukua idara na kuwa kabidhi viongozi wenzao waliotuleta hadi hivileo....


(1)....Mh:Judith Mtawali Kuanzia ..mwaka 1993 hadi 1997
Mkurugenzi wa Uhamiaji,

(2)...Mh:Kinemo D. Kihomano...Mwaka 1997 hadi 2010
Mkurugenzi wa Uhamiaji,

(3)...Mh.Magnus P. Ulungi...Mwaka 2010.............

nivyema tuwajue na kuwakumbuka kwa kazi yao nzuri walio ifanya mara tu baada ya Uhuru hadi hivileo....Tuna wapongeza sana....................................................................

SENENE...wa mkoani Kagera

MWAE ziwani victoria
  Napenda kukitambulisha kivutio hiki cha ajabu katika ziwa letu hili la la Victotia haya ni mawe makubwa yaliyo jipandikiza juu ya mawe haya makubwa yenye uvutio mkubwa katika ziwa hili la victoria tukiweza kusema yakuwa Tanzania tumepata upendeleo mkubwa kutoka kwa Mungu mawe haya ni sehemu ndogo tuu ya kivutio hiki katika ziwa hili lililo sheheni samaki wakubwa, aina ya Sangara, Terapia, na wengine wengi waliomo ndani ya ziwa hili lakini kwaleo ningependa kukutambulisha kisiwa kilicho pombezoni mwa mwalo wa Bukoba kijulikanacho kwa jina la Kisiwa cha  KEREBE, kisiwa hiki kipo usoni mwa mji wa Bukoba na ukisimama katika kiwanja cha ndege cha Bukoba utakiona kikijitokeza kwa upanda wa kushoto mwa uwanja huu

KEREBE: na mialo ya mji huu wa Bukoba ni mazalio makubwa wa panzi hawa maarufu wajulikanao kwa jina la SENENE senene ni aina ya panzi wanao kuja kwa msimu wa majira ya mvua zinazo nyesha humu mkoani kwaetu Bukoba na kagera kiujumla panzi hawa wamekuwa wakipewa hesima kubwa kwa wenyeji hawa wa mkoa huu wa kagera wameweza kutumika kama zawadi kutoka kwa Mungu na wamekuwa wakitumika kwa kutumiana aidha kwa watu wapenda nao kuonyesha hali ya kukuthamini wewe utumiwao...zawadi hii hufungwa katika majani ya migomba ilio andaliwa vizuri na yenye kutoa mvito kwa utumuwae.

SENENE: mara watakapo pokelewa kwa mtumiwae na yeye alie kabidhiwa atapaswa kurudisha shukurani kama vile kanga, kitenge na kadharika

BUKOBA: mara senene hao wakamatwapo hutayarishwa kwa kuchemshwa na kuanikwa kwa muda mpaka watakapo kauka na kuhufadhiwa ....lakini kunawengine hutolewa mabawa na kuwekewa viungo mbalimbali ili kuongeza radha kwamfano pilipili, kitunguu/ kitunguu saumu binzari nk. hii ni katika kuongeza radha tuu kiujumla ni burudani tipu huko mkoani kwetu KAGERA njoo ujionee vijimambo vya mkoa huu wa Kagera.

Saturday 20 April 2013

MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI...

SIMBA
 Hivi kwenye ukweli kwanini uongo usijitenge huyu bwana ni mfalme wa poli na alipokea sifanyingi sana za kolini na binadamu yakuwa yeye ndiye mfalme wa poli wengine walimwita nikiboko wa njia akivimba hapapitiki au wengine walidai yakuwa hawezi kuzoeleka na kutu chochote na hawezi kuchekewe na kiti chochote.....aaaaaaa! huo ni uongo msemakweli ni mpenzi wa mungu hebu tazama sasa mfalme wa poli akichezewa sharubu na huyu simba jike kwahiyo ile dhana yakuwa huyu bwana ni kuboko ya wote ni uongao nayeye ana kiboko yake .....na hawezi kufurukuta katika mahusiano haya yaliyo pangwa na mungu ....hatamimi na wewe hakuna awezae kujua dhana hii imepeperushiwa wapi kati wa hahasimu hawa wawili kwakweli ajuaye ni mola tuu kwa kweli fumbo hili ni lazima tumuachie mungu hivyo nivyema tumjiue mungu kwania yeye ndiye mfumbuzi wa yote
KIBOKO

Sasa ona mwanadamu alivyo kuwa mnafiki ni muda mchache alikiri yakuwa simba ni kiboka wa yote hivi kwa hili ni nani wa kupongezwa yakuwa ni msema ukweli sasa kiboko ni mnyama mpole sana na ameamua kumfungia kazi mwanadami na kumwonyesha nayeye anayawezi...".KWAKWELI YOTE YANAWEZEKANA MBELE YA MUNGU"

KIJIJINI KWETU....Mandera , Kwamagome....ya Tanga

ndugu na jamaa -kijijini Mandera
 Matembezi yangu mkoani Tanga nilitembelea kijijini kwangu Mandela na Kwanmagome Handeni Tanga nilikaruibishwa na nduguzangu , jamaa marafiki wote walifurahia ujiu wangu na kukumbushana mengi ya miaka ya nyuma iliyo pita tulitembelea maeneo ya kijijini kwetu , tulisalimiana na ndugu tulikunywa na kula kwa pamoja.....





KIJIJI CHA MANDELA  KIPO WAPI? HUKO MKOANI  TANGA?
Kakweli kijiji cha Mandera kipo Mkoani Tanga Wilaya ya Handeni kijiji cha Mandera na ukitaka kukikifikia itakibidi utoke mjini Handeni na uwe ukielekea njia ya kwenda Korogwe itakuchukia kati ya dakika 30 au 4
kijiji cha mandera
 45 kukifikia kijiji hicho unapotoka Handeni utaelekea stendi ya Chogo ambayo ni stendi ya mabasi ya Handeni utakwenda moja kwa moja hadi ukitane na njia panda mpya ya kutokea Chanika ya Handeni ineyo unganika na ya kwenda Korogwe utakwenda kwa muda wa dakika kadhaa ndipo utakapo iona barabara wa vumbi upande wa kushoto ukiwa ukielekea Korogwe utapinda na kuendelea na njia hiyo ya vumbi kwa muda wa takribani wa dakika 15 niyo ukutane na kijiji hicho cha MANDERA sasa ukienda mbele zaidi utajikuta ukielekea kijiji kingine cha KWAMADULE huko ndiko wazaza wangu waliko tokea.....kijiji hiki kilisifika sana kwa kuwatoa wazee walio tumikia selikari ya awamu ya kwanza wakiwemo walimu askari na wakuu wa idara nyingine nyeti katika nchi hii .....huo mti unao uona ndipo palipokuwa mji wetu wa zamani
kijiji cha kwamagome

...Kijiji cha kwamagome tilipata bahati ya kuku tembelea nako tulipata mapokezi ya kufa mtu tulikula na kunya kwa pamoja na kufurahia ndhari nzuri ya kijijini kwetu kwamagome nikweli " MKUMBUKA KWAO SI MTUMWA"...Nawakaribuisheni kijijini kweti HANDENI......Mjioneee.

NENO NGARA MAANAYAKE...

Mingara
Poli la kimisi lipo mpakani mwa wilaya ya karagwe ukielekea wilaya ya Ngara kabla ya kufika njia panda ielekeayo Ngara, na mpakani mwa Tanzania na Rwanda-Rusumo, utakutana na njia panda ya Benako hapo utakuwa umeingia walaya ya Ngara njia huu ya benako kuelekea Rwanda inapirika pirika nyingi za ujenzi wa taifa utakutana na magari mengi ya mizigo abiria, na hata ya binafsi yanayo ingia na kutoka Ngara kuelekea Rusumo au yanayotokea Rusumo kwenda Ngara.......lakini kwanini nimependa kisemea hili? mimi binafsi nimevutiwa sana na Hadithi hii ya wenyeji wa Wilaya hii ya Ngara ambao walinihabarisha kuhisiana na Neno hili la mji huu wa Ngara kumbe lina maana ya mti mmoja unao onekana katika Wilaya hii ya Ngara mti huu unahesimiwa sana wenyeji wa wilaya hii wajulikanao kwa kabila la, wahangaza na si mwingine bari ni Mngara huu mti una matawi yaliyo jiachia kama mwamviri na yenye majani madogo madogo yanayo onyesa sura nzuri ya mti huu uliotoa jina la wilaya hii ya Ngara.....ukitaka kujua mengi Tembelea Ngara ujionee....


Barabara inayokatisha pori la kimisi mbele kidogo upande wa kilia kama unaelekea Ngara utaliona ziwa chamchuzi ziwahili linapakana na nchi ya Rwanda,
Pori la kimisi
hapo ukiambaa na mpaka wetu huu utakutana
na maporomoko ya maji eneo la RUSUMO.
au Rusumo foll's.....hapa najaribu kukupa picha na kutaka kuku habarisha chanzo cha Mto Kagera
ulipo patia jina hili ni mkoana Kagera..makutano haya utayapatia Katika daraja linalo unganisha,
nchi ya Rwanda na Tanzania pale pana maporomoko sasa muungano wa Mto Ruvuvu, Na Akanyaru....Mto Ruzvuvu mto huu unatokea Nchini Burundi Kupitia pembeni kidogo na Kabanga na Rulenge....Mto Akanyaru hutukea ndani ya Rwanda na yete miwali inakuja kukutana maeneo ya Rusumo ....na kuangukia darajani Rusumo mbelekidogo tuu mto huu hubadilika jina na kuitwa Mto kagera .....mto huu maji yake hubadirika rangi na nikutokana na yanaku tokea mvua zikunyesha Rwanda Akanyaru unaleta maji mekundu......Mvua zikinyesha Burundi Ruvuvu utaleta maji meusi haya ndiyo maajabu ya mto kagera yanapo tokea....njooo ijioneee.

Friday 19 April 2013

kagera sugar...kagera sukari


KAGERA SUGAR-(KAGERA SUKARI)

TUNAPO SEMA:- Kagera Sikari au Kagera sugar ni kampuni ya utengenezaji sukari mkoani kwatu KAGERA…. kwakweli nimepaswa kulisema hili kwakuwa kumekuwepo na dhana ya kuwa mambo mzuri yote yapo mijini… kwakweli usemi huu ulifutwa na marafiki zetu kutoka Australia na mwingine kutoka marekeni ambao walidiriki kusema yakuwa.
 kuwanda hiki cha sikari Tanzania ni hazina ya utajiri iliya jificha katika kiza kinene”  mimi nilifanikiwa kumuuliza kwanini unasema hivi?
   wao wakanijibu “unasikia rafiki ….wewe hujui” kwani nitakueleza na wewe utaamini ….unajua kiwanda hiki kinatumia fedha nyingi katika kuanda sukari tu…  wakacheka na kusema “sukari tuuu” wakaendekea kusema huku wakiwa makini zaidi hiki kiwanda mimi nakuapia ni pesa tupu pesa peesa pesa tupu, alisistiza huku akiashiria kuomba apatiwe kiberiti cha kuwashia sigareti yake….akaanza kutujuza huku… akiiwasha sigareti yake….ona

Unafahami katika mua kunautajiri mwingi sana kwa mfano:-
ü  Muwa:- tuu yale majani yake…..utapata chakula cha wanyama kama vile Ng’ombe, Sungura, farasi, mbuzi, nk. Alisema mmoja wa marafiki hawa alisema,
ü  Molases:-aliemdelea  kusema hii ipo katika aina ya tope zita lenye rangi nyeusi likiandaliwa vizuri lingeweza kutoa spiriti nyingi sana ambayo mngeweza kutengenezea vinywaji vikali ambavyo vinge tengenezwa kitaalamu na vitawaburudisha wananchi, isitoshe pia mahospitarini spiriti hii ingefaa, sasa ona wangepata pesa ningi watakapouza nje ya nchi hivi mnaonaje marafiki sisi tulikaa kimya tukimkodokea macho akaemdelea kusema.
ü  Mbolea:-aliendelea kusema unajua matakataka waliozalishwa na utengenezwaji wa sukari au ya miwa hii ingeweza kusindikwa kwa muda furani hadi yakawa mbolea ambayo yangetumika katika kukuzia mazao ya mashambani na katika bustani zetu za mboga au maua kitu ambachu watu wangegombania na kuwaingizieni fedha nyingi mifukoni mwenu rafiki aliendelea kuelezea.
ü  Gasi:-aliendelea kusema yakuwa hii miwa na uchafu wake ukiuhifadhi kitaaram unaweza kupata gesi nyingi ambayo mngeweza kuitumia katika matinizi yenu kama ya kupikia na hata kuwashia taa katika vijiji vyenu,
ü  Vinywaji:-alisisitiza kwa kusema yakuwa mimi napenda sana kunywa juisi hapa kunaaina nyingi za vinywaji, tangu vya baridi hadi vya moto! Alicheka na kutuomba tumruhusu aendelee na safari yake.

Tulishikwa na butwa tusielewe la kulichangia katika mazungumzo hayo tuliwaaga marfiki zetu hawa na kuendelea na safari yau kurudi kwao….kwakweli mashamba ya Kagera sugar, kimwonekano ni hazina kubwa mkoani kwetu kagera na nikivutio kikubwa sana sana kama hauamini ngojea nikitumie japo picha hizi nawewe uweze kuburudika kama sisi wenzio tunavyo farijika na hazina hii tuliyo nayo huku kwetu Kagea……leo nakuonyesha kwa kiasi tuu sikunyingine nitakuonjesha hata sukari yetu ya Kagera sugar….