Saturday 22 June 2013

mabilioni ya fedha nchini Uswisi



 mabilioni ya fedha nchini Uswisi


JINI KOLELO
 "KATIKA HALI YA KUTISHA JINI KOLELO LAAPA KUWAANGAMIZA WAHUJUMU UCHUMI WA TANZANIA"

Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.

dkhoseaHabari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge.

 Jaji Werema alipoulizwa  maendeleo ya uchunguzi huo, alisema kuwa kazi hiyo bado inaendelea.
“Uchunguzi huo unaendelea,” alisema Werema huku akisita kueleza kwa undani juu ya kazi hiyo kwa kile alichosema kuwa hana sababu ya kufanya hivyo kwa sasa.
“Subiri uchunguzi bado unafanywa,” alisema Werema na alipotakiwa kueleza utamalizika lini alisema: “Utamalizika tu.”
Mwanasheria huyo wa Serikali alikataa kutaja baadhi ya majina ya watu ambao tume yake imewahoji mpaka sasa.
Alisema anashangazwa na swali la namna hiyo, kwa maelezo kwamba ni jambo ambalo liko wazi kuwa ni kinyume na maadili kuwataja watuhumiwa wakati huu uchunguzi ukiwa bado unaendelea.
Uchunguzi huo unafanyika baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mwezi Juni, 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini humo.
Orodha hiyo iliorodhesha pia baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola196 milioni ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni.
Jarida la kimataifa la uchunguzi la The Indian Ocean Newsletter toleo la hivi karibuni, lilimnukuu Werema akisema uchunguzi huo kwa sasa unatia matumaini.
Werema anaripotiwa akiri kuwa uchunguzi huo umefikia ‘hatua ya kutia matumaini’ na wanaendelea na kazi hiyo kwa uangalifu ili kuwa na uhakika wa taarifa wanazozitafuta.
Alisema kwamba taarifa ya awali inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na tayari idadi kubwa ya wahusika wakiwamo wabunge wameshahojiwa.
Werema alisema wanaendelea na uchunguzi kuwabaini zaidi ya Watanzania 200, waliotajwa kuficha mabilioni ya fedha nje ya nchi.
Mbali na Werema, tume hiyo inaundwa na viongozi kadhaa wa taasisi nyeti kama vile Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu.
Tume hiyo inawahusisha pia Mkuu wa Sheria wa BoT, Mustapha Ismail na maofisa kutoka idara ya upelelezi na ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa jarida hilo la kimataifa, miongoni mwa watuhumiwa hao ni wanasiasa na majenerali wastaafu wanaotuhumiwa kutorosha zaidi ya Dola 133 milioni mwaka 2005, kupitia Mfuko wa Ulipaji Madeni ya Nje (EPA)
Baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika wamehojiwa kutokana na taaluma zao, familia zao, akaunti zao za benki zilizoko nchini na nje ya nchi pamoja na nchi walizotembelea mara kwa mara kwa miaka mitatu iliyopita.
Lengo la kuwahoji inaelezwa ni kutaka kujua iwapo walifuata njia zinazotakiwa katika kufungua akaunti hizo nje ya nchi na iwapo fedha zilizohifadhiwa huko zilipatikana kihalali.
Sakata la kashfa hiyo liliibuliwa Bungeni kwa hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe mwishoni mwa mwaka 2012.
Zitto alisema kwamba kiasi cha fedha kilichofichwa nchini Uswisi ni kikubwa zaidi ya hicho kilichotajwa.
Bunge liliipa Serikali kipindi cha mwaka mmoja ambacho kinaishia Oktoba mwaka huu, iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti hiyo bungeni.

WATANZANIA TUJIUNGENI PAMOJA KUYAKEMESAHA HAYA


SELEKALI IMECHOSHWA NA UTUKUTU
WETU SISI WANASIASA

JIHESHIMU UHESHIMIKE …..AMANI YA TANZANIA  ITALINDWA KWA 

NJIA ZOZOTE ZILE

Kupitia kauli ya wazili wetu mkuu alivyo tuasa, mimi nafikiria ni moja ya maaso ya mwisho kwa mtu mzima aidha alie choshwa na utukutu wetu sisi wana siasa ambao bado tume nga’nga’nia kushikilia mna kuabudu uana siasa wa kizamani wa kutukanana kushabikia vurugu mauaji na hata kuunda chuki ndani ya jamii na kuwaacha matajili wetu ambao ni wananchi tunao washawishi kutuchagua tuingie katika mchakato wa kutuwakilishia madai ,
matakwa yetu huko Mjengoni(BUNGENI) sasa mchakato huo unakuja katika picha hii inayo toa picha mbaya yenye kututia kichefu chefu sisi wananchi kwakweli na sisi sasa tunaona ni vyema kwa kauli ya wazili mkuu aliyo itoa huenda ikawa na uzito na yenye kututia uchungu sana sisi wananchi……kila kukicha kuna jitokeza kauli katika vyombo vya habari na tunasikia yaliyo jiri katika anga la walalahoi ambao ndio wanao ombwa kura kwa vipigo, kudharirishwa, kuchaniwa mavazi yao waliyo yanunua  kwa shida ….pia mabomo nayo hayako nyuma yanapenya mpaka ndani ya vyumba vyetu na yakitudhuru sisi wapenda amani,  wakezetu watoto wetu pia wajukuu zetu kwetu sisi wananchi tupendao amani na eti kisa ni wanasiasa wanaowania kwenda mjengoni (BUNGENI) au UDIWANI hivi huko mjengoni (BUNGENI) au ADIWANI hivi himo mjengoni BUNGENI  kutakuwa eneo la kudaiwa hakizetu za maendeleo sisi walalahoi  au litakuwa  eneo la kutekeleza vyisasi, kukomoana, kuzushiana chuki baina ya serekali, wananchi ambao ndio walala hoi, wabunge wenye kuitakia meme walalahoi wa Taifa hili la Tanzania ambalo… lilikuwa Taifa lenye amani utulivi, humu duniani sasa basi WAZILI WETU MKUU KASEMA hakuna mjadala, mjadala tutaupata kwa wahusika watakao lishughulikia hili jee? na tukiwa sisi wapenda amani tutatii maagizo ya serekali na kudai haki zetu kwa ustarabu au tusubili kichapo kutoka kwa wadogo zetu, watoto wetu na hata wajukuu zetu ……

“WATANZANIA TUJIUNGENI  PAMOJA KUYAKEMESAHA HAYA YANAYO ENDELEA KATIKA KULIGAWA TAIFA LETU HILI AMBALO NI KISIWA CHA AMANI”

RIPOTI ZA WANANCHI: 
 
Arusha: Mashuhuda wa tukio la mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki iliyopita Jijini Arusha, wamedai kumwona na kumtambua mtu aliyehusika na tukio hilo lakini wanasema walishidwa kumkamata kutokana na “kushambuliwa kwa risasi na polisi”.
Mlipuko huo ulitokea katika Viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani jijini humo na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi zaidi ya 100.
Mashuhuda hao ambao wote walijeruhiwa kwa risasi wanasema mlipuaji wa bomu alikuwa amevalia shati la kijivu lenye mistari myeusi na suruali ya jeans yenye rangi ya blue na kwamba wajihi wake ni mtu wa kimo cha kati.
Mmoja wa mashuhuda hao ni mlinzi katika Kikosi cha Ulinzi cha Chadema (Red Brigade) ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alidai kwamba alimwona mtu aliyerusha bomu mara tu baada ya tukio hilo.
Mlinzi huyo ambaye alipigwa risasi za mguuni na kifuani wakati akimkimbiza mtu huyo, alisema bomu hilo lililipuka mara tu baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia na kushuka jukwaani.
“Baada ya Mwenyekiti Freeman Mbowe kushuka jukwaani, nikawapanga walinzi kwa ajili ya kuwalinda viongozi waliokuwa wakichangisha fedha. Ghafla nikasikia mlipuko, sikujua ni nini, lakini kuna mama mmoja alikuwa karibu yangu akanionyesha mtu aliyelipua, akisema yuleee…” alisema na kuongeza:
“Alikuwa amevaa shati la kijivu lenye mistari myeusi na suruali ya jeans ya blue. Ni mtu wa kimo cha kati. Watu walianza kumkimbiza kuelekea upande wa Magharibi wa Uwanja kwenye nyumba za NHC. Tuliruka uzio alipopita yule mtu, mara nikasikia risasi imenipata mguuni.”
“Tulikuwa na uwezo wa kumkakata yule mtu, lakini nikaona risasi zimezidi upande wetu nikaona nigeuze na hapo hapo nikapigwa risasi ya kifuani, nikaishiwa nguvu, sikuweza kufahamu mtu huyo alikoishia. Nilijikongoja na kurudi uwanjani.”
Mlinzi huyo ambaye amelazwa katika moja ya hospitali za jijini Arusha anasema alilazimika kuhama hospitali ya Seliani alikokuwa amelazwa awali baada ya kuandamwa na polisi. “Nilikaa siku tatu hospitalini bila kupata huduma yoyote, lakini kila siku madaktari walikuwa wakinihoji maswali,”alisema na kuongeza:
“Mwisho nikaambiwa kwamba nitahamishiwa ghorofa ya chini, nilipouliza sababu wakasema eti Waziri Mkuu atakuja kuniona… Niligoma mwisho daktari akaniambia kuwa kuna polisi waliovaa majoho ya udaktari ndiyo waliotaka nihamishwe”.
Maelezo yake yanafanana na yaliyotolewa na majeruhi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Alila ambaye alisema kuwa alimwona mtu aliyelipua bomu “akiingia kwenye gari la polisi”.
“Baada ya mlipuko, sikujua kama nimeshapigwa risasi, lakini niliona watu wakimkimbiza mtu baada ya mama mmoja kusema kuwa ndiye aliyerusha bomu.
Watu waliokuwa wakimkimbiza walikuwa wakirushiwa risasi na polisi. Baadaye nilimwona mtu huyo akipanda gari la polisi. Nashangaa tena kusikia polisi wakimtafuta huyo mtu,” alisema Alila.

Polisi wodini
Mbali na taarifa kwamba polisi walikuwa wakizunguka katika wodi za wagonjwa wakiwa wamevalia majoho ya madaktari, pia mgonjwa mwingine amedai kwamba askari wamekuwa wakimfuatilia kila kukicha.
Peter Mshanga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Selian hivi sasa kutokana na kujeruhiwa kwa risasi katika mguu wake wa kushoto alisema awali alipelekwa katika hospitali ya St. Elizabeth lakini alihama baada ya kuandamwa na askari kanzu.
“Mara baada ya bomu nilipelekwa Hospitali ya St. Elizabeth na huko nilishangaa kuwaona askari ninaowafahamu wakizingira kitanda changu. Hata nilipokwenda chooni askari mmoja alinifuata, nikamuuliza anataka nini, yeye akanijibu eti anataka kunisaidia, nikamkatalia akatoka nje,” alisema Mshanga na kuongeza:
“Waliendelea kuzingira kitanda changu kwa siku kadhaa, siku ya tatu daktari akasema nitakiwa nihamishiwa hospitali ya Mount Meru, nikapinga”.
Wakati huo walikuwa tayari wameandaa ambulance (gari la wagonjwa) na gari la polisi ili wanihamishe. Ndugu zangu walipinga ndipo nikahamishiwa hapa Seliani,”anasema.
Kuhusu kujeruhiwa kwake, Mshanga alisema baada ya mlipuko alishtukia ameshajeruhiwa mguuni na akaanguka chini.
“Nilikuwa nimeshika Sh500 mkononi nikisubiri kutoa sadaka yangu. Mara nikaona watoto wanaanguka mbele yangu, nikasikia kishindo kikubwa, kisha nikakimbia kubeba mmoja wa watoto, na mimi nikaanguka, kumbe nilikuwa nimejeruhiwa,” alisema.
Jana gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas kuzungumzia suala la polisi kuwafuatilia majeruhi lakini alipopokea simu alisema hawezi kuzungumza kwa wakati huo kwa kuwa yuko kwenye kikao. “Niko kwenye kikao,” alisema Sabas na kukata simu yake.
Mkanganyiko wa taarifa
Wakati Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi ikitoa kauli kuwa polisi walijihami kwa kuwapiga wananchi risasi na mabomu ya machozi, mmoja wa maofisa polisi aliyekuwa uwanjani wakati wa mlipuko ambaye pia hakutaka jina lake litajwe gazetini amekanusha kupiga watu risasi. “Mimi ndiyo nilikuwa pale uwanjani, baada ya bomu kulipuka wafuasi wa Chadema walianza kutushambulia tulipojitokeza kubeba majeruhi hadi wakavunja kioo cha gari yetu. Niliwaamuru askari warushe risasi hewani, hakuna hata mtu mmoja aliyepigwa risasi,” alisema na kuongeza:
“Unajua wafuasi wa Chadema wamelishwa chuki na viongozi wao, kama Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye alisema akivamiwa na majambazi heri afe kuliko kumpigia simu RPC. Ndiyo maana watu walijawa chuki wakaja kutushambulia.”
Aliendelea: “Baada ya kuona mashambulizi yamezidi tukaondoka, lakini baadaye tukarudi na kukuta majeruhi wote wameshaondolewa na wafuasi wa Chadema. Baadhi ya askari kanzu waliwafuatilia majeruhi ili kujua majina na idadi yao ili tutoe taarifa”.
Kama ni risasi basi wamepigwa na viongozi wa Chadema kwani maganda mengi ya risasi yameonekana kuwa ya bastola na viongozi wao wengi wanazo,”alisema.”



“WATANZANIA TUJIUNGENI  PAMOJA KUYAKEMESAHA HAYA YANAYO ENDELEA KATIKA KULIGAWA TAIFA LETU HILI AMBALO NI KISIWA CHA AMANI”

Friday 21 June 2013

UTAFITI MDOGO KUHUSIANA NA VYANZO VYA VURUGU


UTAFITI MDOGO KUHUSIANA NA VYANZO VYA VURUGU ZINAZO
ENDELEA NCHINI TANZANIA…1961…..2013 TO 2015


Naomba kujaribu kuchangia malalamiko ya vitendo vinavyo endelea nchini kweti Tanzania na kusababisha ntafariku wa hali ya juu na kuweka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake katika kipindi kigumu, kiutendaji pia ningependa kukumbushia hali ya wananchi kujichukulia sheria mikonono na kuua watu kwa tuhuma mbalimbali, kwamfano za wizi, ujambazi, uchawi. Nk

Hatikuishia hapo tukaingia kuwashambulua vyombo vya dera kwa mfano ya Police, Wnajeshi, Mgambo, na hata walinzi wa jadi…wakiwemo sungusngu pia kilisiku kukicha ni chuku chuki chuki,

Haya tukaingia masuala ya Kisiasa viongozi wengi wa vyama vya siasi, viongozi wa kidini, watu maarufu, viongozi wa familia, viongozi wa maidara mbali mbali humu nchini tumeona wakidharirishwa, kwa kupigwa, hadi wengine kupoteza uhai wao,
Tazama pia waandishi wa habari wamekuwa ni kero kubwa wawapo kazini kwani utaona kama tuliyo yaona yakitokea lakini yote tuna vilaumu vyombo vya dora kuwa havifanyi kazizao kiumahili kuzuia adha hii.
Hapa tumejaribu kuona katika mambo haya yanalemea wapi na sikwamba tuko kwa ajili ya kutaka kulaumu kwani mcheza kwao hitunzwa kwa mchezo achezao
” NA HUU UTAFITI HAUHUSIANI NA SHIRIKA LOLOTE BALI SISI WALALA HOI TUMEONA PENGENE NDIO CHACHU AU CHANZO CHA HAYA YOTE”
NAANZA KUWEKA KIMIKOA SUGU:
MOROGORO. ARUSHA, KILIMANJARO, MTWARA, LINDI, MARA. MUSOMA, KAGERA, DAR-ES-SALAAM, TABORA. TANGA, MWANZA, MBEYA, IRINGA, ZANGIBAR, PEMBA, PWANI, KIGOMA, SINGIDA

Jedwari hili ni la kubuni
MIKOA
UDINI
UKABILA
SIASA
WAFUGAJI /WAKULIMA
HAKI ZA BIMNADAMU
ASILIMIA
MOROGORO
yah
-
-
yak
yah
15/%
ARUSHA
yah
yah
yah
yah
yah
99/%
KILIMANJARO
yah
yah
yah
yah
yah
99/%
MTWARA
yah
-
yah
-
yah
70/%
LINDI
-
-
-
-
-
0/%
MARA
yah
yah
yah
yah
yah
98/%
SHUNYANGA
yah
yah
yah
yah
yah
45/%
KAGERA
yah
yah
yah
yah
yah
77/%
D’SALAAM
yah
-
yah
-
yah
100/%
TABORA
-
yah
yah
yah
-
30/%
TANGA
yah
-
yah
-
-
50/%
MWANZA
yah
yah
yah
yah
yah
99/%
MBEYA
yah
yah
yah
yah
yah
100/%
IRINGA
yah
yah
yah
yah
yah
60/%
Z’BAR
yah
yah
yah
-
yah
100/%
PEMBA
yah
yah
yah
-
yah
70/%
PWANI
-
-
yah
-
-
03/%
KIGOMA
yah
yah
yah
-
yah
45/%
SIGIDA
-
-
yah
yah
-
30/%




































Ufunguo:
·         Yah…..”upo”
·         -………..”hakuna”
·         %...........asilimia,

Mikoa inayo kidhili kwa matatizo na tunge omba itupiwe macho ni ili yenye pasenti zifuatazo: 100/%...hadi 50/%

Sababa za machafuko:
Ø  Udini,
Ø  Siasa,
Ø  Ukabila,
Ø  Ukiukaji haki za binadamu,
Ø  Migogoro ya wafugaji na wakulima-(arthi)



TUNAOMBA MUNGU ATUONDOLEE MIFARAKANO HII!!!!