Monday 27 May 2013

Waliofeli kidato cha nne

Katibu mtendaji NECTA

 

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako 

  • Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.


Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.

Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.

Matokeo ya awali ndiyo chimbuko la kupitiwa upya baada ya wadau kuyalalamikia na kumlazimisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume ya kuyachunguza Februari 23, mwaka huu.
Kabla ya tume hiyo kuhitimisha shughuli zake, ilitoa taarifa ya awali ambayo ilipendekeza kufutwa kwa matokeo hayo kwa maelezo kwamba Necta ilitumia kanuni mpya ya kukokotoa matokeo bila kushauriana na wadau.
Serikali ilitoa taarifa bungeni kwamba imeamua kufuta matokeo ya 2012 na kuamuru yapangwe upya kwa kufuata madaraja yaliyotumika mwaka 2011.
Ratiba ya Bunge
Wakati hayo yakiendelea, ratiba ya vikao vya Bunge la bajeti imefanyiwa marekebisho na kusogeza mbele zamu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo awali, ilikuwa imepangwa kusoma hotuba yake ya makadirio ya matumizi leo, badala yake nafasi hiyo imepewa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wizara ya Elimu sasa imepangiwa kuwasilisha hotuba yake Juni 4 mwaka huu, hatua ambayo inatajwa kwamba lengo ni kusubiri kutangazwa kwa matokeo hayo ya kidato cha nne na kidato cha sita.
Wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipokutana na wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma, walisema hawako tayari kujadili hotuba ya wizara hiyo hadi matokeo ya kidato cha nne na sita yatakapotangazwa.

Sunday 26 May 2013

DIWANI KAKUNYU-aridhishwa na utafutwaji maji kijijini

DIWANI -MTAALAM WA MAJI
 Kijiji cha Bugango yasakwa chanzo cha maji ya kina kirefu Idara ya Uhamiaji yapongezwa kwa juhudi zake za kukiwekea kituo hiche cha uhamiaji Bugango Maji ya kisima cha kina kirefu kijijini hapo Diwani wa Kata ya Kakunyu afurahishwa kwa jitihada za Idara hiyo na kusema "kama kweli maji yatapatikana basi kijiji hiki kitaondokana ns shida ya maji ....Diwana Richard Bekomize akimpongeza mtaalamu wa uchimbaji wa visima vya umbali mrefu na kuahidiwa yakuwa lazima maji yapatikane hapa.....
MTAALAM WA MAJI-BUGANGO





Mtaalamu wa maji akipima uwepo wa maji katika eneo hili na kudai yakuwa maji yapo bora tupate vipimo vilivyo sahihi na kusema vipimo vyetu ni vyakisasa na msiwe na wasisi kwani shughuli hizi ni za kitaalam tuu

WAPANDA PIKIPIKI WAKABIDHIWA VYETI

Mkuu wa mkoa wa Kagera
Katika hali ya kufurahisha na yakutia moyo Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstahafu Masawae atenga gugango kwa kishindo huku akija na kauli mbiu ya Bugango na amani upendo na maendeleo akiyazungumza hayo katika mahafali ya kuhitimu kwa wapanda pikipiki wapatao 130 waliojitokeza katika mafuzo ya taklibani ya yasio pungua wiki moja na ushwee mkuu wa mkoa alilipuka kwa furaha na kusema hajawahi kuona eneo lililopendelewa na mungu kamahili la Bugango, Kakunyu, Bubale. kwani kilaeneo ni lakijani akasisitiza kwa kusema yakuwa hatamfumbia macho mtu yeyote MWANGO, MFITINI, NA MVURUGAJI WA AMANI.......Kihaya wauita URUGAMBO, BISHUBA, OMUNWA..........alisisitiza yakuwa mambo hayo yanarudisha nyuma maendeleo ya mkoa wa Kagera... asisitiza wananchi wa kagura kupambana na kilimo kwani maendeleo ya kilimo hayawezi kupatikana bila juhudi na maalifa, na kuwaagiza maafisa ugani wa eneo hili kupambana na magonjwa ya mnyauko ambayo huenda yakawa yame vanmia kijiji hiki cha Tarafa ya Kakunyu......

alitoa pongezi nyingi kwa wahitimu ya mafunzo hayo ya pikipiki na kutoa pongezi kwa wakufungi wa mafunzo hayo na kusema yakuwa juhudi zote hiza za kufanikisha mafunzo haya pia yanatokana na msaada mkubwa wa wakina mama ambao ndiyo nguzo muhimu wa kijiji hiki.....

Saturday 25 May 2013

SIKU YA SABATO

SABATO
Siku ya leo ni alfajiri ya ajabu najisikia mwenye nguvu na nilie jaa bashasha mwenye amani rohoni mwangu na siku hii ya yumapili nime shawishika kuingia tena katika nyumba ya bwana leo siku ya sabato kuyakumbuka na kuyafuta yote yaliyo ugubika moyo wangu na kusababisha moyo wangu kuwa mzito wa kuikumbuka nyumba ya bwana .....najikuta katikati ya waumini wa kikristu na nitayari nimo ndani ya kanisa huku nikiwa nimepiga magoti katika eneo nililo lichagua mimi mwenyewe lakini sinta mtendea haki molawangu alie nipa ujasili na kunikumbusha kurudi katika kundi la wanakondoo waasi wa kanisa huenda yeye ndiye aliye nichagilia nikae katika eneo lile .......najikuta nikikumbuka kupiga alama ya msalaba na kutamka kwajina la baba, la mwana laroho mtakatisu amina.....nikaendelea kujiongoza katika sala ya toba mimi mwenyewe.....nikaendelea tena ....kusali sala maarufu ya kikristu ya kumtukuza mama yetu sala ya salamu mama malia hadi nikaimaliza isitoshe nikaendelea kwa kusali kwa sala ya Baba yetu uliyembinguni....nilipo maliza ....nilifurahi sana na kujisikia moyo wangu wenye amani katika ukristu nanilijipongeza kwa kusema Amin 

kukumbuka kwangu kanisa sikwamba mimi ni mtumwa wa dhambi bali nilishindwa kujipangia siku zangu kiusahihi kiasi nilijikuta nimetingwa na mambo ambayo mabo mengine hayana maana katika dunia hii mbayo bwana wetu yesu kristu alitukomboa kwa shida kubwa hadi kuteswa msarabani na kupoteza maisha yake kwa ajili yetu sisi hivyo tunapaswa sisi kuliona au kuona utukufu wa bwana unavyo yafanya miujiza yake mbele ya hekaru la bwana yesu kristu......naomba kuitukuza siku ya bwana na kusema amin.NA MBALIKIWE SANA..

Bugando -Border


Watoto wa shule ya byakateba watembelea Ofisi ya Uhamiaji Bugango Bolder wafurahia kupiga picha ya pamoja wadai wangependa kuwa maaskali mara wamalizapo shule kufikia elimu ya juu

wasema wangependa kujua mengi kuhusian na shughili zinazo fanywa na Ofisi hii


wasema siku wakiwa wakubwa wangependa kusafiri duniani pote na kujifunza mengi kuhusiana na dunia inavyo kwenda


MAPENZI SABUNI YA ROHO















 HIVI KUNAUKWELI KATIKA HILI???????????????????


Ukimuuliza binti yeyote mwenye ndoto ya kuolewa,,akutajie sifa za mume ampendae,sifa ya "awe mpole" itakuwa ktk orodha ya mwanzo kabisa.Ktk utafiti binafsi sifa hii imetajwa na wasichana 74 ikiwa ya kwanza,,wasichana 113 ikiwa ya 2.Lakini kwa wanawake walio ktk ndoa,,wanawake 20 walisema wanapenda mume mpole ikiwa sifa ya 1 na 42 waliobaki waliitaja ikiwa ya 2
Huo ni utafiti binafsi ambao ulitaka kujua tu UPOLE WA MWANAUME una nafasi gani kwa mwanamke

 Lakini kwa nini wanawake au mabinti hupenda mwanaume mpole? Kwa nini mkorofi hatajwi kabisa? Je ni kweli ni watu wanaohitaji huruma kiasi hicho? Mtaalamu wa masuala wa mahusiano wa kimarekani Baruck Miller aliyetafiti mahusiano kwa miaka zaidi ya 20,,anasema "... Mwanamke anampenda mwanaume mpole ili AJITAWALE KTK MAHUSIANO..."

 Siku zote,mwanamke anapenda awe huru kwenda apendapo au kupewa atakacho.Hivyo anapokuwa mbele ya mwanaume mpole hana wasi,,wala hana tabu ya kutimiziwa shida yake.Akikutana na mwanaume mpole sana kiasi cha kukaribia ujinga basi atamuendesha mume/mpenzi kama rimoti control.

 Jambo wanalosahau wanawake ni kuwa,,upole wa wanaume wengi wanautafsiri kama ujinga,uzezeta au kuliona kundi hili la kuchuna wapendavyo.
Laiti wangekumbuka kuwa mwanaume mpole ni kama volcano tuli,,ikilipuka imelipuka basi sifa ya upole ingekuwa ya mwisho.

MWALIMU MJASILIA MALI......

Mwalimu aliyejitoa muhanga kuishi porini

Mwalimu Salvius Nindi (40)  wa shule ya msingi  Mkenda iliopo mpakani wa Tanzania na Msumbiji akiwa katika moja  ya nyumba zake za kitalii anazojenga kwaajili ya kuboresha kipato chake.
mwalimu huyo haonyeshi masikitiko wala kusita pale alipopangiwa kufundisha katika mazingira ya porini kama ambavyo walimu wengine hukumbia na kuacha kazi wakipangiwa katia maeneo yenye mazingira magumu. yeye anadai kuwa ukiyazoea mazingira magumu na kuyakubali yatakubadirisha maisha yako kama ambavyo yeye alitumia mapori kwa kilimo na sasa ni mfanyabishara mkubwa na anaipend akazi yake.
yeye anawashauri walimu wenzake kutokwepa mazingira magumu kwani kazi ni popote kinachotakiwa tu kuwa wabunifu kulingana na mazingira na kujishughulisha na kazi za ziada badala ya kutegemea kipato cha kazi pekee.
Hata hivyo mwalimu huyu anaishauri serikali kuwafikiria zaidi kwa posho walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu ili kuwatia moyo.

LAKUVUNDA HALINA UBANI..

Hadithi ya lakuvunda halina ubani lengo la kusema hivi ninamaana yakuwa kwanza kabisa maana ya maneno haya mawili yanaendana lakini jee kama hayaendani yamnapaswa yaweje tukichukulia nono hili la lakuvunda

 peke yake lina maanicha kitu kilicho vunda, ama kitu kilicho haribika kwamfano kuku alie kufa na kukaa kwa muda furani huharibika hapa utaona yakuwa kavunda na kuanza kutoa harufu mbaya.....ndivyo hivyo hivyo ya kuwa Halina hapa pana maana yakua kisicho hatia hakuna kitu.....tukimalizia kusema

ubani hapa pana maana yakuwa yakuwa harufu nzuri harufu kwamfano ya udi au manukato mazuri kitu kinacho vutia puani chenye kusafisha hewa iwe na manukato......

Lakuvunda halina ubani : katika hadidhi hii nimependa kulitumia kama neno la heshima firani kwa muhusika furani sasa nikiwa na maani yakuwa kitu kilicho haribika au kilicho oza lazima kiwe na harufu ya uozo lakini hiki nilimaanisha lengo ziri yakuwa kilichooza lazima kiwe na harufu lakini hapa namaanisha yakuwa japo kitu kulichooza lazima kiwe na harufu mbaya lakini hiki hakina harufu ....

Lengo na nia ni kuiambia yakuwa unapofanya jambo zuri au baya lazima litaenziwa kama lilivyo na litapendeza machoni mwa watu au lita kirihisha Tendo ni laaina moja lakini kinacho tazamwa ni mantiki ya jambo hilo katika jamii....'mtu furana kacheza mpira kiumaili na kupatia goli wahasika wapenzi wa timu ile washabiki watamsifia kwa kusema fulani bwana mwanaharamu sana kaucheza mpira ule kiumahili hadi kutupatia gori'.....lakini tafsiri hii ukiitumia tofauti italeta maana tofauti umekunywa mapombe yako na kumiminika matusi kisa mashabiki wampira mbona wana yatumia maneno hayo machafu uwanjani....hii si sawa kwani sifa yako haita futika utabakia kimuonekano katika jamii kuwa huna maana tofaiti na yule mshabiki aliye tumia lugha chafu katika jamii lakini alikuwa akishabikia masuala ya mpira atabakia kiuelekeo kuwa yeye ni mshabiki bora na mwenye kuupenda mchezo wa mpira wa miguu.....

hivyo nivyena kujua jambo zuri litabaki kuwa zuru maisha....na jambo baya litabakikuwa baya na lenye kukirihisha na halidumu litatupwa jararani kuoza na kusahaurika....

PAMBANA NA WAGENI WASIO RASMI

 HIVI UNAJUA NI JIKUMU LANANI LA KUPAMBANA NA WAGENI WASIO RASMI TANZANIA? 

Kiujumla mwenye jukumu la kupambana na wageni wasio Rasmi ni jukumu letu sisi sote tangu vyombo vya ulinzi na usalama viongozi wa vjiji, vitongoji, hadi, katika kaya zetu .....nalisema hili kwasababu kumehuwepo na wageni wasio rasmi wengi wanaovuka mipaka na kuingia nchini kiuficho huku wakujua au wakiwa hawajui kutenda hivyo ni kosa

kushindwa kufuata sheria au kupuuzia kufata sheria za Uhamiaji za kuingia ua kutoka nchini na kuripoti katika Ofisi za uhamiaji za nchi husika na kupata huduma za kiuhamiaji kwa kujaziwa Fomu za uingiaji ama za utokaja nchi husika kufanya hivi kingeweza kukusaidia wewe kutojiingiza katika wimbi la wageni wasio Rasmi ambalo limekuwa donda ndugu katika mataifa mbali mbali duniani unafahami vyazo vya kukidhili kwa tatizo hili la wahamiaji wasio Rasmi ni vipi?........

  • Utimizaji wa ndoto za kuishi maisha bora katika maeneo yanchi hisika yaliyo pelekea kwa huyu mtu kuwa mhamiaji asie rasmi.
  • uvamizi wa umakusudi wamaeneo yenye rutuka kutoka nchi moja na kwenda nchi tofauti na ya kwako ya awali.
  • tatizo la ukimbizi.
  • tatila kutojua sheria za nchi moja kwenda nchi husika.
  • matatizo ya kiharifu mhalifu kufanya uhalifu sehemi moja na kuamua kukimbilia sehemu ya nchi ya pili kufanya maficho ili asi bainike.
  • uendeshaji vitendo haramu vikiwemo, ukataji miti mapolini, uwindaji wanyama kwenye hifazi za taifa, uchimbaji madini hovyo bili kufuata taratibu, Ukataji mbao na usafirishaji nje yanchi kihorela, utafutaji kazi bila kufuata kanini taratibu sheria za utumishi wauma......nk

>sasa ni nini cha kufanya ili kupambana na haya yote?
 kimtizamo ni kukata kendelea kuwaficha au kwapa ushirikiano kuwafadhili, au kuwawezesha kukamilisha malengo au ndoto zao..

Madhara yao hawa wahamiaji wasio rasmi ni kuliweka taifa letu rehani kwa kuchaguliwa viongozi wasio wazarendo walio na uchu wa madaraka, mali, na wasio penda maendeleo hivyo wakati umefika wa kusema Wageni wasio rasmi sasa basi na kililinda taifa letu. kwa Upendo na amani .....

Friday 24 May 2013

” TISHIRIKIANENI KUPAMBANA NA UHAMIAJI HARAMU TANZANIA”


 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
JE UNAZIFAHAMU SHERIA ZA UHAMIAJI
Kwakipindi kurefu tumekuwa tukiwaelimisha kuhusu masuala ya kiuhamiaji siku hii yaleo ningependa kukuonyesha vitabu au kanuni zinazo tumika tatika kumuongoza Afisa Uhamiaji, na zinazo mpa uwezo wa kutekeleza majukumu yake nazo zinapatikana katika kitabu hiki ndani yake kuna mikusanyiko ya misahafu hii ifuatayo:

THE IMMIGRATION ACT
(Principal Legislation)
Chapter 54 Revised Edition, 2002

AND

THE IMMIGRATION ACT
(Subsidiary Legislation)
Chapter 54 Revised Edition, 2002
Index to subsidiary Legulation
·         Katika vitabi hivi kuna maelekezo yanayo elekeza kuhusiana na aina ya vibali vinavyotolewa kwa wageni waingiao na kuishi  nchini,….
·         Maelekezo ya mtu asiye hitajika nchini..(PI)…..
·         Aina ya makosa kiuhamiaji……
·         Nini maana ya sheria ya uhamiaji….
·         Uwezo wa kumsamehe…(waziri)……
·         Maeneo ya mipaka ya Tanzania yanao tambulika kisheria…
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
THE TANZANIA  CITIZENSHIP ACT
(Principal Legislation & Act)
Arrangement of sections
CHAPTER 357

·         Kitabu hukina husika san asana na masuala ya Uraia
·         Utaona ninani
·         RAIA WA KUZALIWA…,
·         RAIA WA KURITHI….,
·         TAJINISI…..,
·         NINI MAANA YA KUOMBA URAIA NA HATUA ZAKE…..
·         NAMNA YA KUNYANGANYWA URAIA UA RAIA WA TANZANIA ANAWEZA KUNYANG’ANYWA URAIA….

Aina za Fomu za kujazwa kuombea Uraia…..

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

THE TANZANIA PASSPORTS AND TRAVEL DOCUMENTS
ACT, 2002
Kipo kitabu cha sheria kinacho onyesha aina zote za passport, nani anaestahili kupewa Passport ya Tanzania nk.
Hizi ni aina ya Passport za Tanzania:
Ordinary Passports……………
Service Passport……………..
Diplomatic Passports…….
East African Passport……..
An Emergency Travel document………….
Certificate of Identity……………
Geneva Convention travel documents…………

Taratibu na maelekezo ya utoaji wa passport Garama za malipo zinapatikana katika sheria hizi au ndani ya kitabu huki………wito

” TISHIRIKIANENI KUPAMBANA NA UHAMIAJI HARAMU TANZANIA”

MAKAMANDA WA UHAMIAJI WATINGA BUGANGO

KITUO BUGANGO
Makamanda wa Idara ya Uhamiaji watembelea kituo cha Bugango Border na kufurahishwa na mdhali ya eneo hilo la mpakani watembelea eneo lote la kiwanja cha nyumba na Ofisi ya Uhamiaji iliyo nunuliwa na Idara na kusema "Tumepata eneo zuri la tutendea kazi basi ni jukumu letu kulilinda"

pia awaasa wafanyakazi wa serekali kufanyakazi kwa uadirifu kwani wao ni jicho la idara na serekali kwa ujumla apongeza wafanyakazi kwa kuwepo maeneo hayo na kusema fanyeni kazi kwa uadilifu kwani nyinyi ni jicho la Taifa hili


Mchezo wa pool

Pool
Jee wewe ni mpenzi wa mchezo huu wa pool mimi ni mpenzi sana wa Pool hivi unasemaje kuhusiana na vijana hawa walio buni meza ya pool ya udongo vijana hawa wata weza kutimiza ndoto yao ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mchezo huu

leo nipo kijijini ambapo niliwakuta wamejitengenezea neza ya udongo wa mfinyazi ulio bebwa na fito nyembamba na iliyo wokewa mashimo sita (6) .....mchezo hii wa hapa kijijini unatumia mti mrefu ambao ni fimbo ya kuchezea na mipira inayotumiwa ni ya matunda yajulikanayo kwa jina la Tura kwakweli ukiwaona wakicheza ni burudani tupu

ombi lao kwa wadau kuomba wabau kuingiza vifaa vya mchezo huu nchini kwa wingi ili hata vijana wa kijijini waweze kufaidika kama wenzao wa mjini

dai la kuwa mchezo huu una wapotosha watoto na vijana wengi na kushindwa kuzingatia masuala ya masomo yao walidai si kweli na kuongeza yakuwa mtoto au kijana atapotoka kimaadili kwa kupenda wao wenyewe tutashukuru kama maombi na mawazo yetu yatatiliwa maanani....

Thursday 23 May 2013

Ujuo alama ya sura ya mpaka

Jiwe la Mpaka Tz and Ug
Ukitaka kujua mipaka yetu kuwa ni shwali basi akiliyako itakwenda moja kwa moja katika jiwe hili kwani hii ni Bicon N0 31 iliyopo maeneo ya la Mkakoma huu ni ushahidi unao onyesha utaratibu mzuri wa kuuwekea mpaka arama zinazo onekana kwa vizazi navizazi ukaguzi wa maeneo haya ni wa mara kwa mara kuhakikisha alama za mipaka hii haichezewi na mtu yeyote.....

Bocon hii imejengwa kiustadi wa kurundikea kwa mawe yaliyo shikamani na kuunda kilima cha aina yake hii hutoa picha yakuwa hapo ni mwishoni mwa Tanzania na Nimwanzoni mwa Uganda


Kyaka...Wilaya ya missenyi

Mabaki ya kanisa-"Kyaka"
 > Historia ya ya mabaki ya kanisa hili inarudi nyuma na kutoa tashwira ya uharibifu uliotendwa katika vita vya Nduli Iddi aman Dada,

alidai yakuwa sehemu ya Tanzania ni sehemu ya yanchi ya Uganda na si kwingine bali kwenye mto wa kagera yakuwa ndiyo mpaka baina ya nchi hizo mbili,

Majesi ya Tanzania yenye nidhami ya hali ya juu yalipambana kwa ari kubwa na kuirudisha sehemu ya Tanzania mikononi mwao pia majeshi hayo yalihakikisha Nduli hoyo kutoka katika ramani ya Afrika mashariki na yakati nikweli Nduli Iddi Amini dada alikimbilia    Uarabuni hali hii ilitoa funzo kwa mataifa yote kuwa taifa lenye amani na upendo linauwezo wa kufanya maajabu likijipanga  kimadhubuti kwani Watanzania walikuwa na kila sababu za kumpiga, Nia ya kumpiga walikuwa nayo, na hata uwezo wa kumpiga ulikuwepo......siliyake ulikuwa ni ushindi..

Daraja lenye Hostoria-Tz
>Daraja la Kyaka ni kivutio kikubwa kwa wapita njia kwani historia yake ni kubwa kwa vile darajahili lilikuwa eneo kubwa lililotegemewa kuleta Ushindi kwa majeshi ya Iddi Amini mbinu zilizo tumika hadi kumdhibiti Nduli huyo mimi sinti sema tuiachie historia ishike nafasi yake.
Barabara-Kyaka to Mtukura

.....Barabara itokayo Bukoba hadi Mtukura kwa sasa ni salama imejengwa kwa kiwango cha lami biashara baina ya Tanzania na Uganda yaimarika na ishirikiano wa nchihizi mbili ni wadhati emungu ijalie Tanzania iwe na amani na Maendeleo Amin.

huu si utamaduni wa Kitanzania

uchukuaji sheria mikononi-(mtwara)
> kwakweli mimi sipendi kuonyesha picha hizi kama ni mshabiki wa mpira baina Baselona, au Asenal..bali nikutaka kujia hivi nikipi kitakachi tokea baadae kwani huu utamaduni huu si Wakitanzania bali ni dalili za kujisahau kwani amani tulio kuwa nayo ni kitu adimu sana na huenda kikipotea basi kirudi kitakuwa ni kazi ngumu sana kurudi hebu tutazame mfano huu wa" MAJI YAKIMWAGIKA CHINI SI RAHISI TENA KUZOLEKA" au " TUTAZAME MFANO WA MAZIWA YAKIMWAGIKA CHINI HAYO HAYATAKUWA MAZIWA BORA"

Hivi ninani wa kulaumiwa kwa uharibifu huu wa mali za serikali na za watu binafsi na ninani atakae lipa fidia hii ya mali za wananchi wa Tanzania wasio na hatia

wanajeshi

>Ofisi za serikali ambazo ni mali za wavuja jasho na ni kodi zetu sisi wananchi tunazo katwa kila mwezi hususani kila mwezi tunashindwa hata kuwapeleka shule kutokana na makato makubwa ya kodi na hivi leo mali hizio zina angamizwa kwa ari mpya na kasi ya ajabu kwakweli hii si sawa utamaduni wa Watanzania ni wa kushindana kwa hoja na la si kamtutu wa bubunduki nalisema hili kwasababi wahusika wa kutukia mtutu wa bunduki wapo pembeni wakitukodolea macho huku waktitroti wakisubiri amirijeshi wetu mkuu kuchoshwa na haya tuyatendayo sisi raia

uchukuaji sheria mkononi

Fumanizi
>Kwamasikitiko makubwa napenda kutoa dukuduku langu kuhusiana na utamaduni wa nchi yetu kubadilika badilika kila mara na hasa katika kuuingilia Uhuru wa mahakama hii nipamoja na watu au wananchi kuchukua sheria mkononi na kuviingilia vyombo vya mahakama na vya ulinzi ambao ndiyo wataalamu wa kuvidhibiti vitendo hivyo hususani vya wizi, ujambazi na pia kutoa hukumu kutokana na uzito wa kosa husika .....lakini jamii kosa dogo hitolewa maamuzi mazito hata kugharimu kuutoa uhai wa bina dami ...ona tukio hili la kinyama lililopelekea mpaka watu wazima hawa wakidharirishwa mbele ya hazara na kundi la binadamu wenzao kana nawao hawana makosa  


>Tuone matukikio mengine ambayo yame konga nyoyo za vyombo nya habari Tanzania na wengine wetu wamekuwa wakivishabikia na kuwa kama ni la kwawaida ni pamoja na haya ya ulipuaji wa Makanisa ..kuwauwa watumishi wa kiroho Mapadree, Mashe, isitoshe wananchi kupambana na vyombo vya ulinzi na usalama kwamfano yaliyotokea huko Mtwara, Arusha, Moshi, Mbeya haya yote ni matunda ya kujichukulia sheria mikononi..witowetu kwa sisi wananchi tupendao amani, tunaomba Taasisi za kiroho (kidini),
 wanasiasa, wanazuoni, nk

waanze utamaduni wa kuhubiri  Maendereo, Amani, Upendo, hii iwe ndiyo sara yao kila kukicha kwani huenda hali ikawa mbaya hapo siku za mbeleni ,......wito wetu 'TANZANIA NA AMANI NA MAENDELEO VINAWEZEKANA '

Wednesday 22 May 2013

Mtoto anahaki ya kupelekwa kliniki

kijana Hakizimana
Kijana Hakizimana na mwanawe ni mfano wa kuigwa na vijana wengine huu ni ushahidi tosha yakuwa kunabadhi ya vijana wamekuwa wasikivu baada ya serikali kutamka yakuwa mwanamke anapaswa kusaidiwa baadhi ya majikumu ya kifamilia

kijanahuyu akiwa njiani akielekea Hspitali kuhudhulia Klinika akimsaidia mkewake ambae kwasiku ya leo mama wa mtoto huyu akiendelea na majukumu mengine ya nyumbani ,

anadai yakuwa imekuwa ni tabia yake kumsaidia mkewake katika shunghuli za nyumbani kwa mfano za kupika, kufua, kuogesha watoto kulima nk.

Baba huyu ni wakuigwa na wazazi wengine kwani ulezi wa mtoto unatokea katika upendo wadhati kati ya bwana na mke alitamba kwa kusema yakuwa tayari ameshakuwa na watoto watatu na wote anawapenda kwa dhati....akiniaga alisema kaka ngoja niwahi kwasababu siku yaleo kunadarasa hapo hospitali  tunafundishwa la  malezi bora na familia kwaheri kaka ya kuonana..

magazeti

KENYA: Safari ya Makamu wa rais William Ruto yazua maswali kibao...

- Gharama za kukodi ndege tu, ni TSHS 489,000,000/=
- Wabunge wahoji, wataka kujua sababu za kukodi ndege badala ya kutumia ndege iliyokuwa ikitumiwa na Kalonzo Musyoka

Endelea kusoma hapa..........Magazeti kukusanya taarifa
KENYA: Safari ya Makamu wa rais William Ruto yazua maswali kibao...

- Gharama za kukodi ndege tu, ni TSHS 489,000,000/=
- Wabunge wahoji, wataka kujua sababu za kukodi ndege badala ya kutumia ndege iliyokuwa ikitumiwa na Kalonzo Musyoka

Endelea kusoma hapa -> http://j.mp/13MPi28

Mtwara kwafukuta

Habari zilizoifikia Maisha Times muda huu zinaripoti kwamba hali sio nzuri huko Mtwara, kwa ufupi hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.

Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara wacharuka!


Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam.

Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi)

Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto.

Nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia yachomwa moto.

Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.

Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika.

Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani. (habari haijathibitishwa rasmi)

Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi.

Askari kadhaa wamekufa (habari hii haijathibitishwa rasmi)

Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari kwakuwa wamepita jirani na gari yao.

Yadaiwa askari wengi waliokuja si wa Mtwara, wengi wametoka Masasi na Lindi.

Ving'ora vinalia hovyo. Watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia.

Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari bali vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili Wananchi wayapate.

Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka sasa takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa.

Wakati waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar Kauli mbiu ya Wananchi wa Mtwara ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"

Wananchi walalamikia kituo cha Television na Radio TBC kuzuia na kukata mawimbi yake kutoonekana wala kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa muda. Hatimaye hivi Punde matangazo yarejea.

Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa muda huu Bungeni.
Endelea kuwa nasi mpaka hapo baadae ambapo tutaweza kukujuza zaidi kile ambacho kinaendelea kutukia Mtwara.

Rais wa Marekani Kutembelea Tanzania





Rais wa Tanzania





Rais wa Marekani
Ziara ya Rais wa Marekani Obama kutembelea nchi ya Tanzania inatupa moyo sisi watanzania kwa taifa kubwa kama hili kutudhamini na kuwa na matembezi ya mara kwa mara na si tuu kwa Raisi Obama tuu bali huu umekuwa ni utamaduni wa viongozi wa Marekani kuwa na mahusiano na nchi yetu ya Tanzania kututembelea katika ziara zao za ki serikali lakini si hilo tuu bali katika sekta zote kwa mfano
 Katika masuala ya Kibiashara……….Kielimu………..Kisiasa ndiguzetu hawa wamekuwa mstari wa mbele katika ushirikiano hata hivyo maraisi wa  Marekeni tangu George Bush Klinton….na wengineo wote walikuwa mstari wa mbele katika kuuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Marekeni katika mtazamo huu ni vyema sisi Watanzania kusimama kidete katika kuuimarisha ushirikiano huu  sihilo tuu pia katika kuukaribisha ugeni huu ni vyema kushirikiana na kushikamana kuukaribisha ugeni huu mkubwa na kwa vyama vyote vya siasa itakuwa jambo la busara tuka shikamana hadi dakika ya mwisha kwa kuulinda umoja wetu, amani, na usalama wa wageni wetu hawa watakao kuja kuitembelea nchi yetu ya Tanzania…..Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika….