Wednesday 5 June 2013

Wenye ulemavu waipongeza Tume




Wenye ulemavu waipongeza Tume



Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi Tanzania, imeipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kwa kuwakumbuka watu wenye ulemavu.
Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo, Kelvin Nyema akizungumza na gazeti hili jana alisema, kwa kipindi kirefu jamii ya watu wenye ulemavu walisahaulika na walikuwa hawatambuliki katika maeneo mbalimbali.
“Tumefurahi sana kuona jamii ya watu wenye ulemavu wanaingia katika Bunge kwa kuteuliwa kwani awali uwakilishi ulikuwa hauuwiani na idadi kamili,”

alisema Nyema na kuongeza:
Alisema jamii inatakiwa kutambua kwamba hakuna anayependa kuwa mlemavu hivyo ni wakati wa kuijadili rasimu hiyo kwa makini.

No comments:

Post a Comment