Wednesday 5 June 2013

BUNGENI....WAKILI.




Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

“Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu,
 lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,”

aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

source gazeti la mwanainchi leo.

Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge hilihili la ambalo nae NDUGAI amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa Chifu Adam Sapi Mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini

Mhe NDUGAI akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.

No comments:

Post a Comment