Thursday 20 June 2013

HANDENI DEVELOPMENT GROUP (HDG)





HANDENI DEVELOPMENT GROUP (HDG)
Ni kikundi kipya kinachoundwa mwaka April 2011 chenye wanachama zaidi ya 30 na wote ni wazawa wa Handeni bila kujali makazi yao yalipo,
Kikundi kinajumuisha wafanyakazi na wafanyabiashara mbalimbali wa Handeni.
Kikundi kitafahamika kisheria na kufuata kanuni zote husika.Pia kitajumuisha jopo la wanachama wenye fani husika katika Uongozi,wafanyabiashara,wanasheria,Saikolojia,Dokta(Mifugo/Binadamu),Ualimu,wanauchumi,wahasibu ambao tutashauriana jinsi yakupiga hatua zaidi kimaendeleo kati yetu kama wakazi wa Handeni.
Kikundi hicho kimeundwa kusaidiana kuongeza mwendokasi wa maendeleo mbalimbali kwa wananchi wa Handeni,haswa wanachama wake kupitia mbinu mbalimbali kama wafanyavyo sehemu nyingine duniani.kama;-

  1. i)                    Kuanzisha HDG SACCOS ili wanachama waweze kuweka na kukopa kwa utaratibu maalum kati ya kikundi,bank au taasisi mbalimbali za kifedha.
  2. ii)                  Ushauri malimbali wa kibiashara,sheria,makazi kupitia vikao maalum na website itakayoanza mapema April 2011 hii.(www.handenidg.org)
  3. iii)                Kuwapatia ajira vijana wa Handeni kupitia miradi ya kikundi hiki kutokana na kiwango cha elimu yake.
  4. iv)                Kumsaidia mwanachama katika dharula kama kilio,ugonjwa kwakutoa na kukusanya michango kwa matibabu au mazishi kwa haraka na ikiwezekana hata kwakumkopesha ili kumuondolea tatizo kwanza.
  5. v)                  Kupeana taarifa mbalimbali za matukio ya Handeni kama sherehe(Harusi),na majanga(vifo) kwa walio nje na ndani ya mji wa Handeni.(Nani.Lini,Wapi,Saa ngapi)
  6. vi)                Kusaidiana kwa mikopo kupitia HDG SACCOS na ushauri katika Mipango binafsi kama ujenzi,biashara,ndoa.
  7. vii)              Kurudisha mshikamano/muungano “network” kwa wakazi wa Handeni waliotawanyika sehemu mbalimbali Tanzania na nje ya nchi.
  8. viii)            Website itakuwa na sehemu yamatangazo kwaajiri yatakayo tangaza nafasi za kazi zinazotokea Handeni na itatoa nafasi yakujitangaza kwa kuweka CV yako na maelezo mafupi.(labour market).
  9. shamba la maharagwe
  10. ix)                Kufanya kitu chochote cha maendeleo ya wilaya bila kujari faida ya kikundi kila mwaka.

MALENGO YA BAADA YA MWAKA MMOJA WA KIKUNDI.
Kufungua miradi mikubwa yakukuza kipato cha kikundi kama;-


Ngo'mbe wa kisasa
            KIUCHUMI,
  • o   Kununua eneo kubwa kwa ufugaji wa kisasa na kufungua “butcher” letu binafsi.
  • §  Kuku wakienyeji na kisasa (Mayai na Nyama)
  • §  Mbuzi na G`ombe (Nyama na Maziwa)
  • §  Mifugo mingine kama Bata, Kanga

No comments:

Post a Comment