Friday 7 June 2013

MAUMAU NA WAKOLONI NGOMA DROOO?




MAUMAU NA WAKOLONI NGOMA 
 DROOO?

 



 
Leo serikali ya Uingereza inatarajiwa kutangaza kiwango cha pesa itakayotoa kuwalipa FIDIA WAPIGANIA UHURU wa Kenya kwa mateso waliyopitia chini ya utawala wa kikoloni. 

Ni baada ya miaka mingi ya baadhi ya waliokuwa wapaigania uhuru wa Kenya MAUMAU kudai Uingereza kuwalipa fidia pamoja na kuomba msahama.

Sasa shinikizo hizo zimezaa matunda baada ya mahakama kuamua kuwa manusura hao wana haki ya kulipwa na Uingereza.

Waathiriwa hao huenda wakalipwa shilingi laki tatu za Kenya ambazo ni takriban dola 2,700 kila mmoja. 

Je unadhani kiwango hiki cha pesa kinatosheleza kwa mtu aliyepitia mateso aina yoyote yaliyofanywa na wakoloni?

Je unaona hatua hii kama mwanzo wa wapigania uhuru katika nchi zingine Afrika kudai fidia kutoka kwa wakoloni kwa mateso waliyopitia?

"Na je mkoloni anapaswa kweli kudaiwa au ni serikali zilizopokea mamlaka kutoka kwao zinapswa kuwajibishwa"?

Tuwasilieni.

No comments:

Post a Comment