Sunday 21 April 2013

SENENE...wa mkoani Kagera

MWAE ziwani victoria
  Napenda kukitambulisha kivutio hiki cha ajabu katika ziwa letu hili la la Victotia haya ni mawe makubwa yaliyo jipandikiza juu ya mawe haya makubwa yenye uvutio mkubwa katika ziwa hili la victoria tukiweza kusema yakuwa Tanzania tumepata upendeleo mkubwa kutoka kwa Mungu mawe haya ni sehemu ndogo tuu ya kivutio hiki katika ziwa hili lililo sheheni samaki wakubwa, aina ya Sangara, Terapia, na wengine wengi waliomo ndani ya ziwa hili lakini kwaleo ningependa kukutambulisha kisiwa kilicho pombezoni mwa mwalo wa Bukoba kijulikanacho kwa jina la Kisiwa cha  KEREBE, kisiwa hiki kipo usoni mwa mji wa Bukoba na ukisimama katika kiwanja cha ndege cha Bukoba utakiona kikijitokeza kwa upanda wa kushoto mwa uwanja huu

KEREBE: na mialo ya mji huu wa Bukoba ni mazalio makubwa wa panzi hawa maarufu wajulikanao kwa jina la SENENE senene ni aina ya panzi wanao kuja kwa msimu wa majira ya mvua zinazo nyesha humu mkoani kwaetu Bukoba na kagera kiujumla panzi hawa wamekuwa wakipewa hesima kubwa kwa wenyeji hawa wa mkoa huu wa kagera wameweza kutumika kama zawadi kutoka kwa Mungu na wamekuwa wakitumika kwa kutumiana aidha kwa watu wapenda nao kuonyesha hali ya kukuthamini wewe utumiwao...zawadi hii hufungwa katika majani ya migomba ilio andaliwa vizuri na yenye kutoa mvito kwa utumuwae.

SENENE: mara watakapo pokelewa kwa mtumiwae na yeye alie kabidhiwa atapaswa kurudisha shukurani kama vile kanga, kitenge na kadharika

BUKOBA: mara senene hao wakamatwapo hutayarishwa kwa kuchemshwa na kuanikwa kwa muda mpaka watakapo kauka na kuhufadhiwa ....lakini kunawengine hutolewa mabawa na kuwekewa viungo mbalimbali ili kuongeza radha kwamfano pilipili, kitunguu/ kitunguu saumu binzari nk. hii ni katika kuongeza radha tuu kiujumla ni burudani tipu huko mkoani kwetu KAGERA njoo ujionee vijimambo vya mkoa huu wa Kagera.

No comments:

Post a Comment