Wednesday 17 April 2013

CHAKULA CHA KITANZANIA...UGALI KWA MCHICHA



CHAKULA CHA KITAMZANIA

Napenda kukitambulisha chakula hiki kitamu cha Kitanzania hapa pana ugali, listi nyama, Dagaa wa kupwaza ….. mchicha ugali mweupe uliopikwa kwa kiasili wa Kitanzania maandalizi yake ni vyepesi tuu tukianzia kwa uandaaji wa ugali:

UGALI:  Andaa unga mweupe wa kutosha andaa maji ya moto mekoni (jikoni) baada ya maji kuchemka weka unga kwenye maji yanayo chemka anza kusonga hadi unga na maji yachanganyike na unga ule ulio uweka katika maji yale yalio chemka na kukuonyesha mchanganyiko ule umekamilika na kukuonyesha yakuwa mchanganyiko ule umeiva kwahiyo huo utakuwa ugali umeiva.


MCHICHA: Andaa mchicha vitunguu, nyanya, Mafuta au karanga tui la nazi tenga mchicha huo jikoni kwa muda utaona maji yakitoka kwenye mchicha ule na mchicha ule kuanza kubadilika na kuwa rangi ya kijani na kujitokeza maji chemsha kwa muda mfupi…..toa mchicha wako jikoni weka sufuria nyingine jikoni weka mafuta, karanga au tui la nazi. Kama ni kwa mafuta kaanga vitunguu weka chumvi kwa muda mfupi weka mchicha changanya hadi urudhike mchanganyiko huu upo sawa hapo itakuwa imeiva…….

DAGAA WA MCHUZI: Tayarisha dagaa wako wakavu kwa kuwakosha na kuwaondoa uchafu wakaange kwa muda mfupi na zisikauke sana weka nyanya vitunguu hakikisha mchanganyiko huo unaiva vizuri hadi kuonyesha mchanganyiko huo umeiva hapo ndipo utakapokuwa mwisho na mwanzo wa kuliwa….tenga vuzuri chakulahicho cha kitanzania na anzakula ni chakula kitamu sana hasahasa ukishushia kwa maji  ya baridi.

No comments:

Post a Comment