Saturday 27 July 2013

Watakiwa kujiandaa na gesi




Watakiwa kujiandaa na gesi

mtambo wa gass




Dar es Salaam. Watanzania wametakiwa kufanya maandalizi yatakayowawezesha kunufaika na uchumi utakaotokana na gesi ili kutorudia makosa yaliyofanyika katika mikataba ya madini iliyopita.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Balozi Mwanaidi Maajar alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya warsha zitakazokuwa zikizungumzia uchumi utokanao na gesi zinazotarajia kuanza mwezi ujao.
Majaar alisema,kuna umuhimu wa haraka kwa Serikali kuandaa sera nzuri zitakazoliletea taifa faida na kwamba maandalizi yanahitajika ni yale ya kuwashirikisha watu wote ikiwamo sekta binafsi, vyombo vya habari na wananchi.
“Hatukuwa tayari kwenye mikataba ya madini hata sasa bado hatupo tayari…Safari hii hatutaki kuachwa na treni kwa sababu bado lipo kituoni hivyo lazima tuhakikishe tunaondoka nalo,”

alisema Majaar.
 Balozi huyo alivitaka vyuo vyote nchini kutoa kipaumbele kwenye masomo ya gesi na mafuta ili kupata wataalamu wazalendo wataoweza kusaidia sekta hiyo badala ya Serikali kuagiza watalaamu kutoka nje.Pia elimu kwa waandishi ilihimizw

No comments:

Post a Comment