Thursday 15 August 2013

WAZIRI MWAKYEMBE AIBUKIA UWANJA WA NDEGE

 
 
WAZIRI MWAKYEMBE AIBUKIA UWANJA WA NDEGE 
 ALFAJIRI SAA 10 KWA KUSHTUKIZA

  Waziri wa Uchukuzi, Dr. Harrison Mwakyembe, ameanza kufanya ziara ya kushtukiza jana saa 10 alfajiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), kuangalia mwenendo mzima wa usafirishaji wa mzigo.

Katika ziara hiyo alitembelea vitengo mbalimbali, kikiwemo cha ukaguzi wa mizigo na abiria pamoja na kitengo cha kamera, ambako hivi karibuni kupita dawa za kulevya za mabilioni. Waziri amefanya ziara hiyo siku tatu baada ya kuahidi kuhakikisha inawatia mbaroni watu wanaojihusisha na usafirisha wa dawa za kulevya kupitia viwanja vya ndege nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja wa Usalama wa JNIA, Clemence Jingu, alikiri kuwa Dr. Mwakyembe alifanya ziara hiyo ya kushtukiza ambapo alioneshwa maeneo pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa uwanjani hapo wakati wa ukaguzi wa mizigo. Aidha Dr. Mwakyembe alitembelea eneo ambalo dawa za kulevya zilizokamatwa Afrika Kusini zilipitia.

Alisema Dr. Mwakyembe aliona hali ya ukaguzi inavyofanyika ikiwa ni pamoja na mitambo inayotumiwa katika eneo hilo na kubaini kuwa dawa hizo zilionekana katika mizigo lakini hakuna hatua zilizochukuliwa hali inayoonyesha kuwa huenda kuna njama zilizofanywa na maofisa waliokuwa wanakagua mizigo hiyo.
Taarifa kutoka JNIA zinaendelea kusema, watendaji wa JNIA walikiri kuwa siku ya tukio eneo hilo lilikuwa na maofisa Polisi pekee kwa kuwa mbwa wanaotumika kubaini dawa hizo walicheleweshwa kufika.


Dr. Mwakyembe ameahidi kuwa “kama sehemu ya wajibu wake wa kulitetea Taifa hili, anajitoa muhanga kuhakikisha Wizara yake inawatia mbaroni watu wanaojihusisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya, kupitia viwanja vya ndege nchini.”

No comments:

Post a Comment