Friday 9 August 2013

Waislamu watakiwa kuenzi maadili

Waislamu watakiwa kuenzi maadili ya dini wakati wote



Chalinze. Wananchi katika Kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo

wameaswa kujiheshimu na kuenzi maadili mema ya kidini kwa miezi yote kila mwaka na siyo wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan pekee.
Pia wameshauriwa kupendana na kushirikiana bila kujali itikadi za kidini, kabila na siasa ili kupunguza migogoro inayochochewa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi.
Rai hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Vigwaza wilayani Bagamoyo, Mohsin Bharwani wakati akitoa sadaka ya vyakula na mafuta ya kupikia kwa wanakijiji wa vitongoji 12 na waumini wa misikiti 14 wa kata hiyo. Watu hao walipatiwa kilo 7,000 za mchele, ngano kilo 250 na mafuta ya kupikia lita 300.

No comments:

Post a Comment