Watakiwa kujiandaa na gesi
mtambo wa gass |
Dar es Salaam. Watanzania wametakiwa kufanya maandalizi yatakayowawezesha kunufaika na uchumi utakaotokana na gesi ili kutorudia makosa yaliyofanyika katika mikataba ya madini iliyopita.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Balozi
Mwanaidi Maajar alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi
ya warsha zitakazokuwa zikizungumzia uchumi utokanao na gesi
zinazotarajia kuanza mwezi ujao.
Majaar alisema,kuna umuhimu wa haraka kwa Serikali
kuandaa sera nzuri zitakazoliletea taifa faida na kwamba maandalizi
yanahitajika ni yale ya kuwashirikisha watu wote ikiwamo sekta binafsi,
vyombo vya habari na wananchi.
“Hatukuwa tayari kwenye mikataba ya madini hata
sasa bado hatupo tayari…Safari hii hatutaki kuachwa na treni kwa sababu
bado lipo kituoni hivyo lazima tuhakikishe tunaondoka nalo,”
alisema Majaar.
Balozi huyo alivitaka vyuo vyote nchini kutoa kipaumbele kwenye masomo ya gesi na mafuta ili kupata wataalamu wazalendo wataoweza kusaidia sekta hiyo badala ya Serikali kuagiza watalaamu kutoka nje.Pia elimu kwa waandishi ilihimizw

No comments:
Post a Comment