Saturday, 27 July 2013

SOMA HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUAGA WANAJESHI SABA WA KULINDA AMANI WALIOPOTEZA MAISHA DARFUR, SUDAN


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa zoezi hilo.
Picha an Ofisi ya Makamu wa Rais


HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUAGA WANAJESHI SABA WA KULINDA AMANI WALIOPOTEZA MAISHA DARFUR, SUDAN  TAREHE 22 JULAI 2013
Mhe. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
Mhe. Balozi Seif Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar;
Mhe Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa;
Waheshimiwa Mawaziri; Jenerali Davis Mwamunyange, Mkuu wa Majeshi yaUlinzi;
Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi Wastaafu;Chief of Staff na Chief of Staff Wastaafu;Majenerali;
Maafisa Wakuu;
Maafisa Wadogo; Askari, Wafanyakazi raia wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa;
Waombolezaji wenzangu;
Familia za Wafiwa;
Mabibi na Mabwana.


Leo ni siku ngumu sana kutakiwa kuzungumza. Ugumuwenyewe unatokana na ule ukweli kwamba siyo siku ya furaha bali ya majonzi na huzuni kubwa kwangu, kwa taifaletu na familia za wanajeshi wetu saba marehemu ambaotumekusanyika hapa kuwaaga. Baada ya sherehe zakutunuku Kamisheni kwa Maofisa wapya katika Chuo chaMafunzo ya Kijeshi, Monduli Jumamosi tarehe 13 Julai, 2013 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange aliniarifukutokea shambulio la kuvizia kwa baadhi ya wanajeshi wetuwalioko Darfur. Kwa kuwa wakati ule mapigano yalikuwayanaendelea, aliniambia kuwa atatoa taarifa zaidi baadae kadri taarifa zitakavyokuwa zinapatikana.
Baadae akanipa taarifa kuwa vijana wetu wamefarikina wengine wamejeruhiwa. Lazima nikiri kuwa taarifahiyo ilinihuzunisha, kunisikitisha na kunikasirisha. Kwa niniwatu wa Darfur wawaue wanajeshi wetu ambaowamekwenda kule kuwasaidia wapate utulivu, ili kunusurumaisha yao, kuwaondolea wasiwasi na kuwawezeshawafanye shughuli zenye tija kuendesha maisha yao. Mojakwa moja sikusita kuamini kuwa waliofanya hivyo ni watuwahalifu.
Tangu uhuru ni sera ya nchi yetu kutetea wanyongedhidi ya ukoloni, ubaguzi, uonevu, dhuluma na 

 

watu wotewalioko katika mazingira hatarishi Afrika na duniani. Njia za Kidiplomasia zilitumika na wakati mwingine JWTZlilishirikishwa. Ndio maana tumeshiriki kwenye vita vyaukombozi katika nchi kadhaa zilizopo Kusini mwa Afrika.Vilevile tumeshiriki katika shughuli za kulinda amani katikanchi mbalimbali zikiwemo Liberia, Sierra Leone na Eritrea.Hivi sasa Jeshi letu linaendelea na jukumu hilo nchiniLebanon, Cote d’Ivoire, Darfur (Sudan), Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Katika nchi zote hizo,askari wetu wanasifiwa sana kwa bidii ya kazi, uvumilivu,uhodari na nidhamu ya hali ya juu. Wakati wote tulipoombwa na kukubali kupelekawanajeshi wetu kutekeleza majukumu hayo, uwezekano wawao kujeruhiwa au kufariki yanafikiriwa kutokea.Wanakwenda kwenye maeneo yenye mapigano hivyohatari hizo kutokea ni jambo linalowezekana. Tahadharizote husika huchukuliwa kuepusha hatari hizo. Ndiyomaana hupewa mafunzo ya kutosha na silaha za kutosha.Hata hivyo hutokea nyakati kukatokea yasiyotarajiwa kamayaliyotokea Darfur. Pia yaliwahi kutokea Liberia.
Kufuatia tukio hilo, nilizungumza na Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa ambaye alinielezea masikitiko yakemakubwa kwa yaliyotokea na kutoa pole zake nyingi. Pia alinieleza kuwa alizungumza na Rais Bashir wa Sudanakitaka wahalifu hao wasakwe, wakamatwe na kuadhibiwaipasavyo. Aidha, nilifanya mazungumzo na Rais Omar AlBashir wa Sudan, ambaye naye alinielezea masikitiko yakena kutoa pole nyingi. Katika mazungumzo yangu naye nilimsisitizia umuhimu wa Serikali yake kufanya uchunguziwa kina wa shambulizi hilo na kuwawajibisha waliohusika. Rais Bashir alikubaliana nami na kuahidi kufanya kilalinalowezekana ili ukweli ufahamike na hatua stahikizichukuliwe.
Sisi kwa upande wetu, Jeshi la Wananchi wa Tanzanialimeunda Bodi ya Uchunguzi inayotarajiwa kuelekea Sudankwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo chashambulizi hilo.
Kwa huko Darfur, tangu shughuli za ulinzi wa amani waUNAMID zianze mwaka 2007 walinzi wa amani 41 kutokamataifa mbalimbali wameuawa na zaidi ya walinzi wa amani 55 wamejeruhiwa. Kwa kweli idadi hii ni kubwa mnoinayohitaji kutafakariwa vizuri na wadau wote. Penginewakati umefika wa kuutazama upya mfumo wa kulindaamani Darfur hasa kuhusu uwezo wa kujilinda na wanajeshiwanaolinda amani. Hapana budi uwezo wao uongezwe ili kupunguza vifo na majeruhi. Narudia kuahidi kuwa rai hiitutaifikisha kwa mamlaka husika katika Umoja wa Mataifana Umoja wa Afrika.
Napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru serikali yaSudan, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwaushirikiano mkubwa waliotupatia tangu kutokea kwa tukiola kushambuliwa kwa askari wetu. Pia nawashukuru nakutoa pongezi kwa Waziri Shamsi Vuai Nahodha, JeneraliDavis Mwamunyange na makamanda na askari wote wa JWTZ, kwa jinsi walivyoshughulikia msiba huu tanguilipopokelewa taarifa ya vifo vya mashujaa wetu hawampaka sasa. Mmewapa heshima kubwa wanaoistahili.Asanteni sana.
Kwa namna ya pekee, narudia kutoa pole nyingi kwafamilia za wafiwa. Nawashukuru kwa dhati kwa moyo waowa uvumilivu na subira. Naomba mfahamu kuwa, mimi naWatanzania wote tupo pamoja nanyi katika kuombolezavifo vya mashujaa wetu. Msiba huu ni wa taifa letu lote nawatu wote wenye kupenda amani duniani.
Daima tutawakumbuka mashujaa wetu na tutaendeleakuenzi na kujivunia kazi zao na mchango wao mkubwa kwanchi yetu na dunia kwa ujumla. Nawaomba sote tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za mashujaawetu mahala pema peponi. Amen.
Kwa Jeshi na wanajeshi wetu wote, napenda kumaliziakwa kuwaasa kuwa yaliyotokea Darfur yasiwakatishe tamaakatika kutimiza wajibu wetu Darfur na kwingineko. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
Yaliyotokeayanatukumbusha kuchukua tahadhari zaidi na kuongezauwezo wa kujihami wa wanajeshi wetu kila wanapotumwakutekeleza jukumu lao.
Asanteni

No comments:

Post a Comment