JK awapa siku kumi na nne majambazi na wahamiaji haramu katika mikoa mitatu kujisalimisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameamuru majambazi na
wahamiaji haramu wote katika mikoa mitatu nchini kujisalimisha katika
muda wa siku 14 kuanzia, Ijumaa, Julai 26, 2013 kabla ya kuanza kwa
operesheni kubwa kuliko zote katika historia ya Tanzania nyenye lengo la
kukomesha ujambazi katika mikoa hiyo na kukamata wahamiaji haramu.
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete |
Rais
Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu amesema kuwa leo ametoa amri kwa
vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini kuanza maandalizii ya
operesheni hiyo na hatimaye kuiendesha katika Mikoa ya Kagera, Kigoma na
Geita.
“Majambazi wanateka magari, wanaua watu
wetu, wanapora mali zao. Watanzania hawawezi kuendelea kuishi kwa hofu,
woga na taabu katika nchi yao wenyewe. Tutawasaka majambazi misituni,
tutawasaka majumbani, tutachimbua ardhini kutafuta hata silaha
zilizofukiwa chini,” amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete ametoa amri hiyo mchana wa
leo, Ijumaa, Julai 26, 2013 wakati alipohutubia wananchi wa mjini
Biharamulo, Mkoani Kagera, kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi
wa barabara ya lami kutoka Kagoma, Wilaya ya Muleba kwenda Lusahuga,
Biharamulo.
Rais Kikwete ametoa amri hiyo kufuatia
matukio ya mara kwa mara na yasiyokuwa na mwisho ya majambazi kuteka
mabasi, kuua watu na kupora mali zadi katika mikoa hiyo, hali ambayo
imesababisha malalamiko ya wakazi wa mikoa hiyo.
Rais Kikwete ameaambia wananchi:
“Tumeamua kukomesha upuuzi huu katika mikoa ya Kagera, Kigoma Geita. Leo
nimetoa maagizo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama – Jeshi la
Wananchi, Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Usalama wa Taifa kuandaa
operesheni maalum, operesheni kubwa kuliko zote tokea tupate uhuru.
Upuuzi huu hauwezi kuendelea.”
No comments:
Post a Comment