Miili
ya wanajeshi saba wa jeshi la Umoja wa Afrika raia wa Tanzania ambao
waliuawa kufuatia shambulio huko Darfur inatarajiwa kuwasili leo jijini
Dar es salaam tayari kwa taratibu za mazishi.
Wakati taratibu za maziko zikiandaliwa mwendesha mashtaka mkuu wa
mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensuda ametoa onyo
kali kuhusu shambulizi la hivi karibuni lililowalenga waangalizi wa
amani kutoka umoja wa mataifa na jeshi la umoja wa afrika huko Darfur
sudan na kusema kuwa linaweza kuhesabika kama uhalifu wa kivita.
Katika taarifa yake akiwa Heague Fatou Bensuda amekumbusha pande zote zenye mgogoro kufahamu kuwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ina mamlaka jimboni Darfur.
Hivi karibuni wanajeshi walinda amani saba raia wa Tanzania waliuawa na wengine kumi na saba kujeruhiwa baada ya shambulizi kutekelezwa na kundi ambalo halijafahamika huko Darfur mnamo tarehe 13 mwezi Julai.

"TUNAWAOMBEA KWA MOLA MILI YA WANAJESHI
WETU ILAZWE MAHALI PEMA PEPONI "
No comments:
Post a Comment