Sunday 15 September 2013

MIMI NASEMA HAPANA....

Zigua Samba, Bondei
wana maombi
Maneno ya mungu
Mini nasema hapana yanayotokea Zanzibar yasihusishwa na imani za kiroho ...lakini nikwasababu gani niseme hivi sisi wakristi, na sisi waislami sisi wite ni watoto wa baba mmoja na mama mmoja si ajabu hivi sasa kumuona Mkristu ao mweislami kutinga (kuingia katuka nyumba za ibada na si ajabu kwa mwislamu kusikika akiimba nyimbo za mapambio za kujifariji au za kujipa moyo....si hilotuu lakini tisiishie hapo hata tukiona yakuwa Mkristu kusimama na ndugu zao wa islamu huku akitamka SALAM-ALEIKUM bila ya ajizi hii ni kutokana na undugu wetu ulio shibika tangu miaka ya Mhela mwana, (miongo ya kale) na si hilo tuu bali pia Ndoa, Mazishi, Shughili za maendeleo, shughuli za kusiasa....Tuna vyama vya kisiasa, vyama michezo, hata vyama vya upatu, vyote hutoona ubaguzi baina ya Wakristu na waislamu...haya katika vyombo vya usafiri, katika Maofisi Nikipandishwa cheo hata sikumoja sijawahi kumsikia aidha Mwislamu, Mkristu, au Mpagani atafumgua mdomo wake na kudai kwanini huyo mwenzangu apendelewe ....LAKINI HEBU TUJIULIZENI HIVI KULIKONI??????

sisi wananchi kwa umoja weto tunapaswa kukikemea kitendo hiki cha kijasusi kinacho endelea cha kuwaangamiaza viongozi wetu wa kiroho bila ya kujali yakuwa awe Mkristu, Mwislamu, Nahata, awe Mpagani kwa pamoja tuwekeni msisitizo kuhusiana na kuwatesa hawa watu wa mungu!!

Kwamana hiyo uma wa watanzania nilazima tupambane na kikundi hiki au vikundi hivi vinavya lenga kutugawa sisi, nyinyi, na hata wao

 "TUWENI NA MSHIKA MANO KUWABAINI WANAO UZA WANAO NUNUA NA WALE WANAO TUMWA KUTENDA UHALIFU DHIDI YA WATU WETU WASIO NA HATIA......"

TUNDI KALI: (Tunaomba serikali ipige marufuku bidhaa hii haraka iwezekazavyo kama madawa ya kulevya)...na atakae bainika kuwa nayo basi vyombo vya ulinzi na usalama vimchukulie hatua..

 BILA YA KUMUONEA AIBU.....Tunatoa pole kwa viongozo wetu wote wa kiroho awe wakikristu au wa kiislamu na hata wa kipagani wafanye kazi zao bila ya kuogopa na walione swala hili ya kuwa ni moja ya changamoto katuka kuifanya kazi zao.

TUNA WASILISHA TAARIFA YA KIONGOZI WA KIROHO...NA YALIYO MSIBU.

"
  • PADRI ALITISHIWA KUUAWA KABLA HAJAMWAGIWA TINDIKALI

    Maadili ya kidini
    PADRI ALITISHIWA KUUAWA KABLA HAJAMWAGIWA TINDIKALI

Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang’amba, aliyejeruhuiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, alitoa polisi kiasi cha miezi mitatu iliyopita kuwa alikuwa anatishiwa usalama wa maisha yake.

Akitoa taarifa hizi, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas Assenga alisema siku za nyuma Padri Mwang’amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.

“Unajua kawaida ya watu wa Zanzibar hufanya mazoezi barabarani, sasa kipindi anapita eneo hilo katika kilima, kuna mtu alimwambia atamfanyia kitu kibaya ambacho hatujui ndiyo hiki au la,” alisema Padri Assenga na kuongeza kuwa “mara baada ya kupewa vitisho hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa Sheha wa eneo hilo na kituo cha polisi.”

PICHANI : Padri Mwang'amba akishuka kutoka kwenye ndege ya kukodi iliyomsafirisha kutoka Zanzibar kuja Dar es Salaam kwa matibabu zaidi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
    Kiongozi w kiroho

    Kazi ya Mungu
     
No comments:

Post a Comment