Saturday 14 September 2013

M23 wameahidi kuendeleza mapambano ikiwa leo hawatafikia makubaliano








M.23
Wawakilishi wa kundi la upinzani la  M23 wanatazamiwa kukutana na maofisa wa Serikali ya Kinshasa leo  katika mji mku wa Uganda, Kampala kwa lengo la kujadili njia za kumaliza mapigano mashariki mwa Kongo.
Rais Kabila alisema juhudi zitafanyika kufanikisha mazungumzo ya Kampala lakini alionya kuwa iwapo mazungumzo hayo hayatafanikiwa jeshi litaendeleza oparesheni dhidi ya waasi.
Juzi Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alifungua
mazungumzo ya maelewano ya kitaifa ambayo yanawashirikisha wapinzani na makundi ya kijamii.
Katika ufunguzi wa kikao hicho cha wiki mbili viongozi kadhaa wa upinzani hawakushiriki huku wakimtuhumu Kabila kuwa anapanga kutawala kwa muhula wa tatu mfululizo kinyume cha sheria.
Kabila ambaye muhula wake unamalizika mwaka 2016 alisema mazungumzo hayo yanalenga kujadili sababu za kudhoofika utendaji kazi wa taasisi za kiserikali, pamoja na mapigano Mashariki mwa nchi hiyo ambayo yalianzishwa na wapinzani wa M23miezi 18 iliyopita.
Mazungumzo hayo ya kitaifa ambayo yalipangwa kuanza mwezi Novemba mwaka jana yalianza katika hali ambayo Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya wapinzani.
Mafanikio hayo yalipatikana kutokana na uungaji mkono wa kikosi cha uingiliaji cha Umoja wa Mataifa.
Wito uliotolewa na viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu wa kuitaka Serikali ya Kongo ikae meza moja na  M23 kwa ajili ya kutatua mgogoro wao, ulipokewa kwa mikono mwili na waasi hao, ingawa wametoa angalizo la kurudi tena kwenye uwanja wa mapambano iwapo watachokozwa.
Awali kiongozi wa kundi hilo la  M23, Betrand Bisiimwa, alipongeza uamuzi huo wa kuwataka wakutane na Serikali ya Kongo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wao ambao umedumu kwa muda mrefu.
Bisiimwa akizungumzia uamuzi huo uliofikiwa hivi karibuni katika kikao kilichoketi Uganda, kilichowashirikisha Rais Jakaya Kikwete, Paul Kagame wa Rwanda, Joseph Kabila wa Kongo, Yoweri Museveni wa Kongo na wengine, alisema kikundi chake kilifanya juhudi kama hizo kwa zaidi ya miezi kumi iliyopita, lakini Serikali ya Kongo iliwapuuza, hivyo kusisitiza kwamba wapo tayari kwa mazungumzo au kuendelea na mapigano.
“Naupongeza wito wa viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu kwa sababu wameona umuhimu wa kuyaokoa maisha ya Wakongomani wa hapa mjini Goma, siku zote amani inatafutwa kwa makubaliano ya kukaa meza moja, lakini ukiamua vita hauwezi kushinda,” alisema Bisiimwa.

No comments:

Post a Comment