Saturday 14 September 2013

Hatutavumilia wahamiaji haramu

Tanzania: Hatutavumilia 

wahamiaji haramu

Tanzania: Hatutavumilia wahamiaji haramuWizara ya Mambo ya Ndani ya nchini Tanzania imetoa tamko kwa wahamiaji haramu kurejea makwao mara moja kwa hiyari, kwani zoezi la kuwasaka na kuwarejesha litaanza wakati wowote kuanzia sasa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi amesema tayari amekabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jukumu la kuwahamisha wahamiaji haramu waliopo katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita. Kauli hiyo ya Dk. Nchimbi imekuja baada ya wiki mbili alizotoa Rais Jakaya Kikwete kwa wahamiaji hao kumalizika. Rais Kikwete alipokuwa mkoani Kagera Julai 29 mwaka huu, alitoa tamko kwa wahamiaji wote haramu waliopo katika mkoa huo na maeneo jirani kufunga virago na kurejea makwao. Wahamiaji hao haramu waliorejea makwao ni kutoka nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Dk. Nchimbi  amesema, wakati wa wahamiaji haramu kurejea makwao ni sasa, kwani Tanzania haitavumilia tena wahamiaji haramu.  Ameongeza kuwa, wahamiaji haramu wanaotaka kuishi Tanzania warejee makwao, kisha wafuate taratibu za kuingia na kuishi Tanzania.

Andika maoni







Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)


No comments:

Post a Comment