Ngwair kuagwa leo
Mwili wa msanii wa muziki, Albert
Mangwea ukipokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana kutoka
Afrika Kusini tayari kupelekwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili. Mwili wake
utaagwa leo Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga
Ngwair alifariki wiki iliyopita
nchini Afrika Kusini alikokwenda kwa shughuli za muziki na mwili wake kuletwa
jana mchana.
Dar es Salaam. ‘Alale pema peponi kamandaaa, alale pema peponi Mangweaaa’
Hayo ni maneno yaliyoimbwa na mamia ya vijana waliokuwa wanasukuma gari
lililobeba mwili wa msanii Albert Mangweha, maarufu kama Ngwair.
Jeneza laMangweaaa |
Ngwair alifariki wiki iliyopita
nchini Afrika Kusini alikokwenda kwa shughuli za muziki na mwili wake kuletwa
jana mchana, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam.
Simanzi ilitanda eneo zima la uwanja
walikojazama mashabiki wa sanaa ya muziki, wengi wao wakiwa vijana wakati
jeneza la Ngweair likitolewa sehemu ya ndani ya uwanja na kuletwa nje.
Vilio pia vilitawala kutoka kwa
ndugu wa marehemu na watu wengine walioshindwa kuvumilia baada ya kushuhudia
jeneza hilo likitolewa nje tayari kwa safari ya kupelekwa Hospitali ya Taifa,
Muhimbili.
Kutokana na wingi wa watu, vijana wa
skauti walilazimika kufanya kazi ya ziada kuunganisha mikono yao ili gari
lililobeba mwili wa Mangwair liweze kupita bila kuzongwa, jambo lililowashinda
nguvu.
Hali ilikuwa tofauti baada ya kundi
la vijana kuendelea kuimba wimbo wa Kamanda, huku wakisukuma gari lililobeba
mwili wa Ngwair na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.
Kadri mwili wa msanii huyo
ulivyokuwa ukisogea mbele, ndivyo watu hasa vijana walivyokuwa wakijitokeza
kutoka pembezoni mwa barabara na kuungana na wengine kusukuma gari.
Kazi ya kusukuma gari hiyo
iliendelea kwa muda mrefu kupita barabara kuu ya Pugu kuelekea Muhimbili,
ambako mwili wake ungehifadhiwa kabla ya kuagwa.
Rais wa Shirikisho la Muziki
Tanzania, Ado Novemba alisema mwili wa marehemu utaagwa leo kwenye Viwanja vya
Leaders Club, Kinondoni kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa sita mchana.
Baada ya hapo, marehemu
atasafirishwa kwenda Morogoro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kwenye
makaburi ya Kihonda.
Awali, mwili wa Ngwair mwimbaji wa kibao
‘Mikasi’, ulitarajia kuwasili mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini ilishindikana
kutoka na sababu za kitaalamu kulazimisha mwili huo kupimwa ili
No comments:
Post a Comment