MAX MELO MAJORITY OWNER WA
JAMIIFORUMS ATOA SHUKRANI YA
AJALI MBAYA ILIYOMKUTA!!
Kwanza
namshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kuishi tena (2nd chance) mimi na mdogo
wangu. Mungu yu mwema kwetu.Katika ajali hii, huwezi kutarajia kuwa tumetoka
tukiwa hai na tunaendelea vema kama tulivyo sasa.Aidha, nawashukuru wote
waliotoa pole zao kwetu via JF na kututakia kupona haraka. Tunashukuru sana na
tunazidi kufarijika kwa ushirikiano wenu katika maombi (na baadhi walituma
michango itusaidie katika matibabu). Moderators, shukrani kwa kuendelea
kulisimamia jukwaa hili kwa weledi mkubwa.Napenda kuwashukuru wanasiasa watatu;
ndugu
Zitto Kabwe, Dr. Faustine Ndugulile na Ndugu Hussein
Bashe
- ambao wameonyesha kujali tangu tunapata ajali hadi sasa (wanatujulia hali
tunavyoendelea); hii inatia moyo na kuonyesha kujali kwao kwetu. Mungu
awazidishie muendelee kuwa na moyo huu.Shukrani zetu ziende kwa wana JF wa
Nzega, Mwanza na Dar; ambao wamekuwa nasi bega kwa bega tangu siku ya ajali. Ni
wengi lakini inakuwa vigumu kuwataja kwenye shukrani zetu hizi bali tunapenda
wafahamu kuwa tunawashukuru sana.Tunawashukuru sana wengine wote ambao kwa njia
tofauti wamekuwa wakitaka kujua tunaendeleaje kiafya na kuwajuza hapa; kutokana
na mazingira tulikuwa tunashindwa kuwajibu wote lakini wengi tumewajibu
kuwafahamisha kilichotokea na tunavyoendelea.Ndugu zangu, tupo hai kwa mapenzi
ya Mungu tu!Nini kilitokea?
Inakuwa
vigumu kuelezea kwa kirefu kilichotokea. Kuwa ni mwendo kasi? Sijui. Kuwa ni
mkono wa mtu? Pia sijui. Kuwa ni bahati mbaya? Naweza kusema hivyo! Hatumlaumu
yeyote katika hili na hatumnyooshei kidole yeyote. Kwa dereva yeyote anafahamu
nini kinaweza kutokea pale 'Sterling Rod' inapokatika ukiwa katika mwendo zaidi
ya spidi 80.Yapo mengi yanaweza kuhisiwa, yapo mengi yanaweza kusemwa lakini
ambacho tunaweza kukiri ni kuwa Mungu yu mwema kwetu.Hali yetu:
Baada ya ajali, mdogo wangu ambaye pia ni member wa JF kama Chachu Ombara, alibainika kuvunjika mfupa wa kati ya kiwiko na bega mkono wa kushoto na sasa amefanyiwa upasuaji na madaktari bingwa Muhimbili, anaendelea vema.Binafsi nilibainika kuwa na uvimbe kidogo kwenye ubongo upande wa kulia; naendelea vema namshukuru Mungu.Mwisho:
Ushauri wangu kwa wanaoendesha magari, wasafiri kwenye ruti ndefu na hata katika hali ya kawaida:
- Kabla ya safari yoyote mwite Mungu na ujikabidhi kwake, atakuitikia kwa namna ya kipekee
- Unapoendesha, funga mkanda. Hata kama umekaa siti ya nyuma (katika gari binafsi).

-
Ukiwa barabarani (dereva), jitahidi kuzingatia alama za barabarani; wajali
madereva wengine kama ambavyo ungependa wakujali.Nasikitika kuwa huenda
nisijibu maswali ambayo labda yanaweza kujitokeza kutokana na kuwa nina
matatizo ya kuumwa kichwa (kilijigonga sana chini wakati gari linapinduka)
lakini naamini nikikaa vema nitarejea na aidha kujibu au nikiwa nimechelewa
nitatuma PM kwa mhusika.Asanteni sana.MaxenceTokana na maoni ya wengi wa wadau wa
Jukwaa La Siasa kutokua na taarifa hii mbaya ya Ajali ilipokua imetangazwa
hapa, mtuwie radhi Moderators kwa maamuzi ya kuhamishia habari hii Jukwaa La
Siasa toka habari na hoja Mchanganyiko. Habari hiyo ya ajali ilipostiwa
hapa na inapatikana kwenye kiunganisho hiki kilicho ambatanishwa -Maxence Melo
apata Ajali mbaya Maeneo ya Nzega.
No comments:
Post a Comment