Je
unalijua Kabila lako vizuri? Haya ni Makabila Yanayopatikana Nchini Tanzania
Kuna matatizo kwenye majina kadhaa katika orodha hii,
kwasababu mbalimbali. Orodha hii inatokana na orodha ya Ethnologue ya lugha za
Tanzania, pamoja na tovuti nyingine. Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya
makabila ni majina ya lugha au lahaja badala ya makabila, na labda majina
mengine yaliandikwa vibaya. Juu ya hivyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema
kwamba kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina
wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vinavyo mamilioni ya watu; labda kila
kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa.
Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na
ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi
tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila
yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani. Orodha hii
haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi kutoka vita
katika nchi za jirani. Ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka
nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Arabia au Uhindi.
Waalagwa (pia wanaitwa Wasi),wanatokea Mkoa wa
Dodoma, Wilaya ya Kondoa. Lugha yao ni Chasi. Waakiek,Waarusha,Waassa,
Wabembe ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma,
Wilaya ya Kigoma Vijijini. Lugha yao ni Kibembe.
Wabena ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa
Iringa, Wilaya ya Njombe.Lugha yao ni Kibena
Wabende ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Rukwa,
Wilaya ya Mpanda. Lugha yao ni Kibende,
Wabondei ni kabila la Tanzania wanaoishi katika
Mkoa wa Tanga, karibu na Milima ya Usambara. Lugha yao ni Kibondei.
Wabungu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mbeya, Wilaya
ya Chunya. Lugha yao ni Kibungu.
Waburunge ni kabila la Tanzania wanaoishi katika
Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa. Lugha yao ni Kiburunge
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi
kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli
kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo. Wachagga wana historia ndefu ya asili
yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa
makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima
Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya Kilimanjaro
Siha, Machame. Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu, Wa-Old Moshi,
Wa-Kibosho, na Wa-Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo,
Wa-Uru, na Wa-Siha.
Lugha
ya Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha
magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika
katika Kirombo, Kimarangu, Ki-Old Moshi,Kikibosho, Kimachame, Kikirua na
Kisiha. Lugha hizi zinakaribia kufanana kulingana na jinsi makabila hayo
yalivyopakana. Kwa mfano, Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua, ambacho nacho
kinafanana kidogo na Kimarangu. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame
ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia
sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika
kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wamachame
ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
Majina
ya Kichagga
Majina
ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si
lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama
Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame.
Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka
Old Moshi na Vunjo. Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe,
Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu,
Makundi, Urasa, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu. Rite, Makule,
Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo,
Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio,
Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.
Wachagga
wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea
wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa
sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi
cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni
pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada
ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.
Wadatooga (pia huitwa Wataturu, Wamang'ati au
Wabarabaig) ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Manyara na Singida.
Lugha yao ni Kidatooga
Wadigo ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Tanga, hasa
kwenye mji wa Tanga. Pia wako Kenya wanapoishi upande wa Kusini wa mji wa
Mombasa. Katika Kenya huhesabiwa kati ya mijikenda. Lugha yao ni Kidigo.
Wadoe ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Pwani,
Wilaya ya Bagamoyo. Lugha yao ni Kidoe.
Wafipa ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Rukwa, hasa
katika wilaya za Sumbawanga na Nkansi. Lugha yao ni Kifipa.
Wagogo (mmojawao anaitwa Mgogo) ni kabila la Tanzania ya kati,
wenyeji wa mikoa ya Dodoma na Singida. Lugha yao ni Cigogo (kwa Kiswahili
hutamkika Kigogo).
Dini
ya wengi wao ni Ukristo, hasa wa madhehebu ya Anglikana, halafu wa Kanisa
Katoliki. Historia ya Wagogo inaweza kuelezeka kwa kuangalia yafuatayo: Utawala
wa jadi, nyumba za asili, chakula kikuu na lafudhi ya lugha. Majina ya ukoo ya
Cigogo
majina
hayo ni kama Mazengo, Cidosa, Cilongani, Malecela, Mwaluko, Mavunde, Ndejembi,
Manyesela, Mbogambi, Mdachi, Kapaya,Matonya, Mtunya, Kusila, Nhonya,Mhalanyuka,
Mbenaa, Chibile, Mdoli,
Lusinde,Njamasi,Majenda,Chiwamba,Mazoya,Ufinyu,Chilyawanhu,Magaya,
Ngoli,Chiwanga,Lubeleje,Makupila,Fukunyi
Waha ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma, pia
mpakani na Burundi. Lugha yao ni Kiha.
Wahaya ni Kabila linalopatikana katika Mkoa wa Kagera, Kaskazini
Magharibi mwa Tanzania, kandokando mwa Ziwa Victoria. Lugha yao ni Kihaya
Wahehe ni kabila la Tanzania ambalo kiasili linaishi katika wilaya
za kaskazini za Mkoa wa Iringa, yaani Iringa, Kilolo na Mafinga.
Ni
moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji. Ndiyo sababu
wanazika wafu wao wakielekea mashariki.
Lugha
yao (Kihehe) imegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi) tofautitofauti
kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na kimaana na lugha
ya Kibena iliyopo wilayani Njombe.
Wajita ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara. Lugha
yao ni Kijita.
Wakaguru ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro,
Wilaya ya Kilosa. Lugha yao ni Kikaguru.
Wakinga ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Iringa,
Wilaya ya Makete. Lugha yao ni Kikinga
Wakuria ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara, pia
wako Kenya. Lugha yao ni Kikuria
Waluguru ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Morogoro na
Pwani, hasa kwenye Milima ya Uluguru. Lugha yao ni Kiluguru.
Waluo (pia Wajaluo) ni kabila hasa la Kenya. Wako pia Uganda ya
msahriki na wachache wanaishi nchini Tanzania katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni
Kiluo. Wenyewe hujiita Jaluo na lugha yao Dhulou.na mengi kuhusu waluo.tembelea
websitehii;www.jaluo.com utacheka mpaka ujambe puuu.ongito nyamwanda 0784334032
en an jakiseru jakanyango
Waluo ni mkusanyiko wa kabila la kinilotiki ambalo lilisafiri
kutoka Afrika ya Kaskazini kufuata mto Nile kuja Kusini. Waluo wengi wameenea
kandokando ya Ziwa Viktoria kutokana na utamaduni wao wa uvuvi. Kwa Afrika
mashariki utawakuta nchini Sudan, Kenya, Uganda na Tanzania.Waluo mashuhuri
Ø
Gidi
Gidi Maji Maji - Waimbaji wa hiphop
Ø
Tom
Mboya - mwanasiasa aliyeuawa 1969
Ø
Barack
Obama - mwanasiasa na seneta wa Marekani ni mwana wa baba Mluo
Ø
Jaramogi
Oginga Odinga - kiongozi wa Waluo wakati wa uhuru, mwanzilishaji wa chama cha
KANU na makamu wa rais wa kwanza
Ø
Raila
Amolo Odinga - mwana wa Jaramogi na mwanasiasa muhimu wa kitaifa
Ø
Robert
Ouko - waziri wa mambo ya nje aliyeuawa 1990
Wamasai ni kabila wazawa wa Afrika la watu wahamaji katika
wanaopatikana Kenya kaskazini Tanzania.
Wamachinga ni kabila la Tanzania wanaoishi katika
Mkoa wa Lindi, wilaya za Kilwa na Lindi. Lugha yao ni Kimachinga.
Kwa
kipindi cha karne ya 21 wamekuwa maarufu katika miji kwa kuuza bidhaa wakiwa
wameshika mkononi wakisaka wateja.
Wamakonde ni kabila la Tanzania wanaoishi katika
Mkoa wa Mtwara. Pia wako Msumbiji. Lugha yao ni Kimakonde.
Wamwera ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, hasa
kwenye Wilaya ya Nachingwea. Lugha yao ni Kimwera.
Wandengereko ni kabila la Tanzania wanaoishi katika
Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Rufiji. Lugha yao ni Kindengereko.Hapana, Wandengereko
hawaishi Mkoa wa Ruvuma bali mkoa wa Pwani kusini ya Dar es salaam katika Wilaya
za Mkuranga na Rufiji.
Wangindo ni kabila la Tanzania wanaoishi upande
wa Kusini wa Tanzania. Lugha yao ni Kingindo,
Wanyakyusa (pia huitwa Wangonde au Wasochile) ni
jina kwa ajili ya watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za
kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) upande wa kaskazini ya Ziwa Nyasa. Lugha yao
ni Kinyakyusa. Mara nyingi Wagonde upande wa kusini ya mto Songwe nchini Malawi
huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.
Kihistoria
watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde na Wanyakyusa walikuwa kabila
kubwa kati yao. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa" imekuwa jina la
kundi kwa jumla. Hadi leo kanisa la kilutheri la KKKT linatumia jina
"dayosisi ya Konde" kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.
Wakati
Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini ya Ziwa Nyasa mwisho wa karne ya 19
hawakuona tofauti ya kimsingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa
sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana na jina lililokuwa
kawaida ziwani.
Leo
hii ni watu zaidi ya milioni wanaojumlishwa kwa jina hili, takriban 700,000
wanaokaa upande wa Tanzania na 300,000 wakikaa Malawi.
Wanyamwezi ni kabila la Tanzania wanaoishi katika
mikoa ya Tabora na Shinyanga. Lugha yao ni Kinyamwezi.
Wasukuma ni kabila kubwa kutoka eneo la kusini
na mashariki ya Ziwa Viktoria, nchini Tanzania. Kabila hili hasa huishi katika
mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Mwaka 2001 idadi ya Wasukuma ilikadiriwa kuwa
3,200,000 [1]. Lugha yao ni Kisukuma. Kisukuma ni miongoni mwa lugha za Kibantu
ambazo hubainishwa kama lugha mabishi.
Wayao ni kabila kutoka eneo la kusini ya Ziwa Nyasa. Mwaka 2001
idadi ya Wayao ilikadiriwa kuwa 1,942,000, ambao 1,000,000 wanaishi Malawi,
450,000 ni wakazi wa Msumbiji, na 492,000 wako Tanzania [1]. Lugha yao ni
Kiyao.
Wazanaki ni kabila kutoka eneo la kaskazini-magharibi ya nchi ya
Tanzaniai,
Wazaramo ni kabila kutoka eneo baina ya Dar es Salaam na Bagamoyo,
nchini TanzaniaWazaramo ni sehemu ya Wabantu. Mababu wanaaminika waliingia
katika eneo la Tanzania katika milenia ya kwanza. Historia yao ya kimdomo
inasema ya kwamba walihamia pwani katika mazingira ya Daressalaam kutoka
Uluguru (Morogoro) katika karne ya 18.
Walipokaa
kwenye pwani walikuwa karibu na makazi ya Waswahili wakaanza kufaamiana na
Uislamu. Taarifa za wakoloni Wajeruami mwanzoni wa karne ya 20 zinaonyesha ya
kwamba wakati ule Uislamu ulikuwa umeenea kati ya Wazaramo na waliendelea
kujiunga nayo haraka [2]. Siku hizi idadi kubwa wa Wazaramo ni Waislamu.
Makabila Mengine Ni Haya Hapa Chini
Wakabwa,Wazigula,Wazinza,Wazyoba,Wahadzabe
(pia wanaitwa Watindiga),Wahangaza, Wakahe,Wakami,Wakara (pia wanaitwa
Waregi),Wakerewe,Wakimbu,Wasumbwa,Waswahili,Watemi(piawanaitwaWasonjo),Watongwe,Watumbuka,Wavidunda,Wavinza,Wawanda,Wawanji,Waware(inaaminikalughayaoimekufa),,Wanyanyembe,Wanyaturu(piawanaitwaWarimi),Wanyiha,Wapangwa,Wapare(piawanaitwaWasu),Wapimbwe,Wapogolo,Warangi(auWalangi),Warufiji,Warungi,Warungu(auWalungu),Warungwa,Warwa,Wasafwa,Wasagara,Wasandawe,Wasangu,Wasegeju,Washambaa,Washubi,Wasizaki,Wasuba,
Wanyambo,Wanyamwanga, ,Wandonde,Wangasa, ,Wandali,Wandamba,Wandendeule,
.Wangindo,Wangoni,Wangulu,Wangurimi (au Wangoreme),Wanilamba (au
Wanyiramba),Wanindi,Wamakua (au
Wamakhuwa),Wamakwe(piawanaitwaWamaraba),Wamalila,Wamambwe,Wamanda,Wamatengo,Wamatumbi,Wamaviha,Wambugwe,Wambunga,Wamosiro,Wampoto,Wamwanga,
,Wamagoma, ,Wakutu,Wakw'adza,Wakwavi,Wakwaya,Wakwere (pia wanaitwa
Wanghwele),Wakwifa,Walambya, Wakisankasa,Wakisi,Wakonongo, Wagorowa (pia
wanaitwa Wafiome),Wagweno, Waikizu,Waikoma,Wairaqw (pia wanaitwa
Wambulu),Waisanzu,Wajiji
No comments:
Post a Comment