SELEKALI IMECHOSHWA NA UTUKUTU
WETU SISI WANASIASA
JIHESHIMU
UHESHIMIKE …..AMANI YA TANZANIA
ITALINDWA KWA
NJIA ZOZOTE ZILE
Kupitia kauli ya wazili wetu mkuu alivyo
tuasa, mimi nafikiria ni moja ya maaso ya mwisho kwa mtu mzima aidha alie
choshwa na utukutu wetu sisi wana siasa ambao bado tume nga’nga’nia kushikilia
mna kuabudu uana siasa wa kizamani wa kutukanana kushabikia vurugu mauaji na
hata kuunda chuki ndani ya jamii na kuwaacha matajili wetu ambao ni wananchi
tunao washawishi kutuchagua tuingie katika mchakato wa kutuwakilishia madai ,
matakwa yetu huko Mjengoni(BUNGENI)
sasa mchakato huo unakuja katika picha hii inayo toa picha mbaya yenye kututia kichefu
chefu sisi wananchi kwakweli na sisi sasa tunaona ni vyema kwa kauli ya
wazili mkuu aliyo itoa huenda ikawa na uzito na yenye kututia uchungu sana sisi
wananchi……kila kukicha kuna jitokeza kauli katika vyombo vya habari na tunasikia
yaliyo jiri katika anga la walalahoi ambao ndio wanao ombwa kura kwa vipigo,
kudharirishwa, kuchaniwa mavazi yao waliyo yanunua kwa shida ….pia mabomo nayo hayako nyuma
yanapenya mpaka ndani ya vyumba vyetu na yakitudhuru sisi wapenda amani, wakezetu watoto wetu pia wajukuu zetu kwetu
sisi wananchi tupendao amani na eti kisa ni wanasiasa wanaowania kwenda mjengoni
(BUNGENI) au UDIWANI hivi huko mjengoni (BUNGENI) au ADIWANI hivi himo mjengoni
BUNGENI kutakuwa eneo la kudaiwa
hakizetu za maendeleo sisi walalahoi au
litakuwa eneo la kutekeleza vyisasi,
kukomoana, kuzushiana chuki baina ya serekali, wananchi ambao ndio walala hoi,
wabunge wenye kuitakia meme walalahoi wa Taifa hili la Tanzania ambalo…
lilikuwa Taifa lenye amani utulivi, humu duniani sasa basi WAZILI WETU MKUU
KASEMA hakuna mjadala, mjadala tutaupata kwa wahusika watakao lishughulikia
hili jee? na tukiwa sisi wapenda amani tutatii maagizo ya serekali na kudai
haki zetu kwa ustarabu au tusubili kichapo kutoka kwa wadogo zetu, watoto wetu
na hata wajukuu zetu ……
“WATANZANIA TUJIUNGENI PAMOJA KUYAKEMESAHA HAYA YANAYO ENDELEA KATIKA KULIGAWA TAIFA
LETU HILI AMBALO NI KISIWA CHA AMANI”
RIPOTI ZA WANANCHI:
” Arusha: Mashuhuda wa
tukio la mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki iliyopita Jijini Arusha,
wamedai kumwona na kumtambua mtu aliyehusika na tukio hilo lakini wanasema
walishidwa kumkamata kutokana na “kushambuliwa kwa risasi na polisi”.
Mlipuko huo ulitokea katika Viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa kuhitimisha
kampeni za udiwani jijini humo na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi
zaidi ya 100.
Mashuhuda hao ambao wote walijeruhiwa kwa risasi wanasema mlipuaji wa bomu
alikuwa amevalia shati la kijivu lenye mistari myeusi na suruali ya jeans yenye
rangi ya blue na kwamba wajihi wake ni mtu wa kimo cha kati.
Mmoja wa mashuhuda hao ni mlinzi katika Kikosi cha Ulinzi cha Chadema (Red
Brigade) ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alidai kwamba alimwona mtu
aliyerusha bomu mara tu baada ya tukio hilo.
Mlinzi huyo ambaye alipigwa risasi za mguuni na kifuani wakati akimkimbiza
mtu huyo, alisema bomu hilo lililipuka mara tu baada ya Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia na kushuka jukwaani.
“Baada ya Mwenyekiti Freeman Mbowe kushuka jukwaani, nikawapanga walinzi kwa
ajili ya kuwalinda viongozi waliokuwa wakichangisha fedha. Ghafla nikasikia
mlipuko, sikujua ni nini, lakini kuna mama mmoja alikuwa karibu yangu
akanionyesha mtu aliyelipua, akisema yuleee…” alisema na kuongeza:
“Alikuwa amevaa shati la kijivu lenye mistari myeusi na suruali ya jeans ya
blue. Ni mtu wa kimo cha kati. Watu walianza kumkimbiza kuelekea upande wa
Magharibi wa Uwanja kwenye nyumba za NHC. Tuliruka uzio alipopita yule mtu,
mara nikasikia risasi imenipata mguuni.”
“Tulikuwa na uwezo wa kumkakata yule mtu, lakini nikaona risasi zimezidi
upande wetu nikaona nigeuze na hapo hapo nikapigwa risasi ya kifuani, nikaishiwa
nguvu, sikuweza kufahamu mtu huyo alikoishia. Nilijikongoja na kurudi
uwanjani.”
Mlinzi huyo ambaye amelazwa katika moja ya hospitali za jijini Arusha
anasema alilazimika kuhama hospitali ya Seliani alikokuwa amelazwa awali baada
ya kuandamwa na polisi. “Nilikaa siku tatu hospitalini bila kupata huduma
yoyote, lakini kila siku madaktari walikuwa wakinihoji maswali,”alisema na
kuongeza:
“Mwisho nikaambiwa kwamba nitahamishiwa ghorofa ya chini, nilipouliza sababu
wakasema eti Waziri Mkuu atakuja kuniona… Niligoma mwisho daktari akaniambia
kuwa kuna polisi waliovaa majoho ya udaktari ndiyo waliotaka nihamishwe”.
Maelezo yake yanafanana na yaliyotolewa na majeruhi mwingine
aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Alila ambaye alisema kuwa alimwona mtu
aliyelipua bomu “akiingia kwenye gari la polisi”.
“Baada ya mlipuko, sikujua kama nimeshapigwa risasi, lakini niliona watu
wakimkimbiza mtu baada ya mama mmoja kusema kuwa ndiye aliyerusha bomu.
Watu waliokuwa wakimkimbiza walikuwa wakirushiwa risasi na polisi. Baadaye
nilimwona mtu huyo akipanda gari la polisi. Nashangaa tena kusikia polisi
wakimtafuta huyo mtu,” alisema Alila.
Polisi wodini
Mbali na taarifa kwamba polisi walikuwa wakizunguka katika wodi za wagonjwa
wakiwa wamevalia majoho ya madaktari, pia mgonjwa mwingine amedai kwamba askari
wamekuwa wakimfuatilia kila kukicha.
Peter Mshanga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Selian hivi sasa kutokana
na kujeruhiwa kwa risasi katika mguu wake wa kushoto alisema awali alipelekwa
katika hospitali ya St. Elizabeth lakini alihama baada ya kuandamwa na askari
kanzu.
“Mara baada ya bomu nilipelekwa Hospitali ya St. Elizabeth na huko
nilishangaa kuwaona askari ninaowafahamu wakizingira kitanda changu. Hata
nilipokwenda chooni askari mmoja alinifuata, nikamuuliza anataka nini, yeye
akanijibu eti anataka kunisaidia, nikamkatalia akatoka nje,” alisema Mshanga na
kuongeza:
“Waliendelea kuzingira kitanda changu kwa siku kadhaa, siku ya tatu daktari
akasema nitakiwa nihamishiwa hospitali ya Mount Meru, nikapinga”.
Wakati huo walikuwa tayari wameandaa ambulance (gari la wagonjwa) na gari la
polisi ili wanihamishe. Ndugu zangu walipinga ndipo nikahamishiwa hapa
Seliani,”anasema.
Kuhusu kujeruhiwa kwake, Mshanga alisema baada ya mlipuko alishtukia
ameshajeruhiwa mguuni na akaanguka chini.
“Nilikuwa nimeshika Sh500 mkononi nikisubiri kutoa sadaka yangu. Mara
nikaona watoto wanaanguka mbele yangu, nikasikia kishindo kikubwa, kisha
nikakimbia kubeba mmoja wa watoto, na mimi nikaanguka, kumbe nilikuwa
nimejeruhiwa,” alisema.
Jana gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus
Sabas kuzungumzia suala la polisi kuwafuatilia majeruhi lakini alipopokea simu
alisema hawezi kuzungumza kwa wakati huo kwa kuwa yuko kwenye kikao. “Niko
kwenye kikao,” alisema Sabas na kukata simu yake.
Mkanganyiko wa taarifa
Wakati
Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera na Uratibu wa Bunge,
William Lukuvi ikitoa kauli kuwa polisi walijihami kwa kuwapiga wananchi risasi
na mabomu ya machozi, mmoja wa maofisa polisi aliyekuwa uwanjani wakati wa
mlipuko ambaye pia hakutaka jina lake litajwe gazetini amekanusha kupiga watu
risasi. “Mimi ndiyo nilikuwa pale uwanjani, baada ya bomu kulipuka wafuasi wa
Chadema walianza kutushambulia tulipojitokeza kubeba majeruhi hadi wakavunja
kioo cha gari yetu. Niliwaamuru askari warushe risasi hewani, hakuna hata mtu
mmoja aliyepigwa risasi,” alisema na kuongeza:
“Unajua
wafuasi wa Chadema wamelishwa chuki na viongozi wao, kama Mbunge wa Arusha
mjini Godbless Lema ambaye alisema akivamiwa na majambazi heri afe kuliko
kumpigia simu RPC. Ndiyo maana watu walijawa chuki wakaja kutushambulia.”
Aliendelea:
“Baada ya kuona mashambulizi yamezidi tukaondoka, lakini baadaye tukarudi na
kukuta majeruhi wote wameshaondolewa na wafuasi wa Chadema. Baadhi ya askari
kanzu waliwafuatilia majeruhi ili kujua majina na idadi yao ili tutoe taarifa”.
Kama
ni risasi basi wamepigwa na viongozi wa Chadema kwani maganda mengi ya risasi
yameonekana kuwa ya bastola na viongozi wao wengi wanazo,”alisema.”
“WATANZANIA TUJIUNGENI PAMOJA KUYAKEMESAHA HAYA YANAYO ENDELEA KATIKA KULIGAWA TAIFA
LETU HILI AMBALO NI KISIWA CHA AMANI”