Wednesday, 11 September 2013

Wanasiasa kikwazo wahamiaji haramu






Dar es Salaam. Wanasiasa jijini wameshutumiwa kutokana na kuingilia mchakato wa kupambana na wahamiaji haramu unaondeshwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Kichefuchefu
chimbuko la wahamiaji haramu
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Said Meck Sadick alisema licha ya mchakato huo wa kupambana na wahamiaji haramu kuendelea vyema lakini wanasiasa hao wamekuwa wakiwakwamisha.
Alisema wanasiasa hao wamekuwa wakifanya mikutano usiku na wahamiaji hao kinyume cha sheria na taratibu na kuwapa moyo wahamiaji hao kuwa wasijali hakuna mtu atakayeweza kuwarudisha kwenye nchi zao.
“Operesheni hii tumeianza tarehe Mosi Septemba mwaka huu, lakini hawa wenzetu wanataka kutukwamisha kwa masilahi yao binafsi tunawaonya waache mtindo huu mara moja,”
 alisema
 Sadick.
 Nakuongeza kuwa;

“Baadhi yao tunawajua na tena wanadiriki kusema kuwa wahamiaji hao niwapiga kura wao ni raia halali wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment