M.23 |
Rais Kabila alisema juhudi zitafanyika kufanikisha
mazungumzo ya Kampala lakini alionya kuwa iwapo mazungumzo hayo
hayatafanikiwa jeshi litaendeleza oparesheni dhidi ya waasi.
Juzi Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo alifungua
mazungumzo ya maelewano ya kitaifa ambayo yanawashirikisha wapinzani na makundi ya kijamii.
mazungumzo ya maelewano ya kitaifa ambayo yanawashirikisha wapinzani na makundi ya kijamii.
Katika ufunguzi wa kikao hicho cha wiki mbili
viongozi kadhaa wa upinzani hawakushiriki huku wakimtuhumu Kabila kuwa
anapanga kutawala kwa muhula wa tatu mfululizo kinyume cha sheria.
Kabila ambaye muhula wake unamalizika mwaka 2016
alisema mazungumzo hayo yanalenga kujadili sababu za kudhoofika utendaji
kazi wa taasisi za kiserikali, pamoja na mapigano Mashariki mwa nchi
hiyo ambayo yalianzishwa na wapinzani wa M23miezi 18 iliyopita.
Mazungumzo hayo ya kitaifa ambayo yalipangwa
kuanza mwezi Novemba mwaka jana yalianza katika hali ambayo Jeshi la
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepata mafanikio makubwa katika
mapambano dhidi ya wapinzani.
Mafanikio hayo yalipatikana kutokana na uungaji mkono wa kikosi cha uingiliaji cha Umoja wa Mataifa.
Wito uliotolewa na viongozi wa nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu wa kuitaka Serikali ya Kongo ikae meza moja na M23 kwa
ajili ya kutatua mgogoro wao, ulipokewa kwa mikono mwili na waasi hao,
ingawa wametoa angalizo la kurudi tena kwenye uwanja wa mapambano iwapo
watachokozwa.
Awali kiongozi wa kundi hilo la M23, Betrand
Bisiimwa, alipongeza uamuzi huo wa kuwataka wakutane na Serikali ya
Kongo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wao ambao umedumu kwa muda
mrefu.
Bisiimwa akizungumzia uamuzi huo uliofikiwa hivi
karibuni katika kikao kilichoketi Uganda, kilichowashirikisha Rais
Jakaya Kikwete, Paul Kagame wa Rwanda, Joseph Kabila wa Kongo, Yoweri
Museveni wa Kongo na wengine, alisema kikundi chake kilifanya juhudi
kama hizo kwa zaidi ya miezi kumi iliyopita, lakini Serikali ya Kongo
iliwapuuza, hivyo kusisitiza kwamba wapo tayari kwa mazungumzo au
kuendelea na mapigano.
No comments:
Post a Comment