Kilimanjaro |
OPARESHEN KIMBUNGA
Bukoba. Serikali imesema wahamiaji haramu walioolewa na Watanzania wanaruhusiwa kubaki nchini, hawalazimiki kuvunja ndoa zao ingawa wanatakiwa kupata kibali maalumu kutoka Idara ya Uhamiaji.
Akizungumza mjini hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa
Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, alisema wahamiaji haramu
walioolewa wanatakiwa kwenda Idara ya Uhamiaji kupata hati hizo.
Rusumo |
Kikosi kazi |
Pia, alisema kwa mujibu wa sheria, mhusika atapewa
kibali alichokiita ‘Independence Pass’
kitakachomwezesha kuendelea kuishi nchini na kwamba, kinyume chake itakuwa ni kuvunja haki za binadamu.
kitakachomwezesha kuendelea kuishi nchini na kwamba, kinyume chake itakuwa ni kuvunja haki za binadamu.
Hata hivyo, Massawe alibainisha kuwa lazima zoezi
la kuondoa wahamiaji haramu lifanyike, kwani walioondoka kwa hiari ni
11,601 na waliokadiriwa kuondoka ni kati ya 52,000 na 53,000, hivyo
idadi kubwa bado wanaishi nchini.
Maafisa Uhamiaji |
Akizungumzia zoezi la kurudisha wahamiaji haramu
lililoanza rasmi Septemba 6, mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma, Mkuu
Msaidizi wa Operesheni hiyo, Simon Sirro, alisema tayari wamewakamata
1,851.
No comments:
Post a Comment