Kilima njaro |
Dar es Salaam. Mwanamke ambaye ni raia wa Nigeria, amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akiwa na kete 99 za dawa za kulevya.
Hata hivyo kete hizo hazikujulikana ni za aina gani.
Kukamatwa kwa raia huyo, kumekuja wiki tatu tangu
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kutangaza vita dhidi ya watu
wanaopitisha dawa za kulevya katika idara na taasisi zilizoko chini ya
wizara yake.
Akizungumza na Mwananchi jana, Meneja Usalama wa uwanja huo, Clemence Jingu, alisema mtuhumiwa alikamatwa jana saa 8:00 mchana
Alisema kete hizo alikuwa ameziweka katika makopo ya poda na mafuta.
“Kete hazijajulikana ni za aina gani, kwa sasa tunafanyika utaratibu wa kutambua aina yake,” alisema.
“Kwa sasa hapa JNIA kuna mitambo ya kisasa ya
kuweza kuwabaini wanaopitisha dawa hizi, tulimkamata akiwa na kete 99,
kati ya hizo kete 30 alikuwa ameweka katika kopo la mafuta ya nywele,
kete nyingine alikuwa ameweka katika kopo la poda za watoto,” alisema.
Unga |
“Baada ya kumhoji ametueleza kuwa dawa hizo
alizinunua maeneo ya Magomeni, kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi
kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano zaidi,” alisema.
Alisema kuwa binti huyo aliingia nchini Agosti 30mwaka huu, akitokea nchini Nigeria.
No comments:
Post a Comment