kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Jumatano na Alhamisi wiki hii, ikiwa ni mwanzo wa mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa utakaotekelezwa kwa kuanzia katika mitihani hiyo.
Taarifa ya Baraza la Mitihani
la Tanzania (Necta), inaonyesha kuwa wanafunzi hao wanatoka kwenye shule 15,677
zikiwamo za umma na binafsi.
Inaeleza taarifa hiyo kuwa,
wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani wa lugha ya Kiswahili ni 844,810
kati yao wasichana wakiwa 444,475 na wavulana 400,335. Kati
ya wanafunzi hao, wasioona ni 88 wavulana wakiwa ni 56 na wasichana 32 huku
wenye uono hafifu wakiwa 546 na kati yao wavulana ni 263 na wasichana 283.
Watakaofanya mtihani huo kwa
lugha ya Kiingereza ni 22,535 na kati yao wavulana wakiwa 11,430 na
wasichana 11,105. Wanafunzi wenye uono
hafifu kati ya hao ni 51, wavulana wakiwa 21 na wasichana 30.
Mwaka jana wanafunzi 894,881
kutoka shule 15,363 walifanya mtihani huo, huku wale waliofanya mtihani huo kwa
lugha ya Kiswahili wakiwa 873,837 wavulana walikuwa 415,572 na wasichana
458,265.
Waliofanya mtihani huo
kwa lugha ya Kiingereza walikuwa 20,457 wavulana wakiwa 10,422 na
wasichana 10,035. Wenye uono hafifu walikuwa ni 45 wavulana wakiwa 26 na
wasichana 19.
Msemaji wa Necta, John
Nchimbi, alilieleza gazeti hili kuwa tayari mitihani imeshasambazwa huku
akionya kuhusu wale watakaojaribu kufanya udanganyifu wa aina yoyote ile.
“Tunawataka wanafunzi na
wadau wote wanaohusika na mtihani huu, wasije wakajihusisha na udanganyifu kwa
namna yoyote ile, Necta tupo makini na tumejipanga kwa chochote
kitakachotokea,” alisema na kuongeza:
“Tunaamini kuwa wanafunzi
wameandaliwa vya kutosha na wao ni vyema wajiandae zaidi kisaikolojia, yeyote
atakayebainika kufanya udanganyifu tutamchukulia hatua zinazostahili ikiwa ni
pamoja na kumfutia matokeo.”
Wanafunzi hawa wanaanza
mtihani wakati ambapo Serikali imeweka lengo la kuinua ufaulu wa mtihani huo
kutoka asilimia 31 za mwaka jana mpaka 60 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Maandalizi ya mwisho
Shule mbalimbali za msingi
zimeshafungwa tangu Ijumaa iliyopita kati ya wiki moja hadi mbili zikiwaacha
wanafunzi wa darasa la saba wakikamilisha hatua za mwisho mwisho kabla ya
kufanya mtihani wao.
Akizungumza jana kwa simu, Mwalimu Mkuu wa Shule ya High Mount
iliyoko Guluka Kwalala Kata ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam, George
Mgombozi alisema: “Kwa sasa tunawajenga wanafunzi kisaikolojia baada ya
kuwapika vya kutosha. “Kimsingi, tunachowaambia wanafunzi ni kwamba
watambue kuwa wanapofanya mitihani yao waone kama mitihani ya kawaida tu
wanayoifanya kila siku,” alisema.
Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi
Mloganzila iliyoko Wilaya Kisarawe Mkoa wa Pwani, Grace Msele amewataka
wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kutumia siku mbili zilizobaki
kujiandaa kisaikolojia na kujiepusha na michezo ya hatari kabla ya
kuanza mitihani yao. Akizungumza kwenye kikao cha wazazi shuleni hapo
juzi, Msele alisema kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuwa karibu na
watoto wao katika kipindi hiki ili kuwajengea uwezo.
Mtoto wa Kitanzania |
No comments:
Post a Comment