Wawakilishi wa kundi la upinzani la M23
wanatazamiwa kukutana na maofisa wa Serikali ya Kinshasa leo katika mji
mku wa Uganda, Kampala kwa lengo la kujadili njia za kumaliza mapigano
mashariki mwa Kongo.
WAPIGANAJI WA... UN |
KIKUNDI CHA... M23 |
Juzi Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo alifungua mazungumzo ya maelewano ya kitaifa ambayo
yanawashirikisha wapinzani na makundi ya kijamii.
Katika ufunguzi wa kikao hicho cha wiki mbili
viongozi kadhaa wa upinzani hawakushiriki huku wakimtuhumu Kabila kuwa
anapanga kutawala kwa muhula wa tatu mfululizo kinyume cha sheria.
Kabila ambaye muhula wake unamalizika mwaka 2016 alisema
mazungumzo hayo yanalenga kujadili sababu za kudhoofika utendaji kazi wa
taasisi za kiserikali, pamoja na mapigano Mashariki mwa nchi hiyo
ambayo yalianzishwa na wapinzani wa M23miezi 18 iliyopita.
Mazungumzo hayo ya kitaifa ambayo yalipangwa
kuanza mwezi Novemba mwaka jana yalianza katika hali ambayo Jeshi la
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepata mafanikio makubwa katika
mapambano dhidi ya wapin
Mafanikio hayo yalipatikana kutokana na uungaji mkono wa kikosi cha uingiliaji cha Umoja wa Mataifa.
Wito uliotolewa na viongozi wa nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu wa kuitaka Serikali ya Kongo ikae meza moja na M23 kwa
ajili ya kutatua mgogoro wao, ulipokewa kwa mikono mwili na waasi hao,
ingawa wametoa angalizo la kurudi tena kwenye uwanja wa mapambano iwapo
watachokozwa.
Awali kiongozi wa kundi hilo la M23, Betrand
Bisiimwa, alipongeza uamuzi huo wa kuwataka wakutane na Serikali ya
Kongo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wao ambao umedumu kwa muda
mrefu.
Bisiimwa akizungumzia uamuzi huo uliofikiwa hivi
karibuni katika kikao kilichoketi Uganda, kilichowashirikisha Rais
Jakaya Kikwete, Paul Kagame wa Rwanda, Joseph Kabila wa Kongo, Yoweri
Museveni wa Kongo na wengine, alisema kikundi chake kilifanya juhudi
kama hizo kwa zaidi ya miezi kumi iliyopita, lakini Serikali ya Kongo
iliwapuuza, hivyo kusisitiza kwamba wapo tayari kwa mazungumzo au
kuendelea na mapigano.
No comments:
Post a Comment