WAZIRI MWAKYEMBE AIBUKIA UWANJA WA NDEGE
WAZIRI MWAKYEMBE AIBUKIA UWANJA WA NDEGE
ALFAJIRI SAA 10 KWA KUSHTUKIZA
Waziri wa Uchukuzi, Dr. Harrison Mwakyembe, ameanza kufanya ziara ya
kushtukiza jana saa 10 alfajiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), kuangalia mwenendo mzima wa usafirishaji
wa mzigo.
Katika ziara hiyo alitembelea vitengo mbalimbali,
kikiwemo cha ukaguzi wa mizigo na abiria pamoja na kitengo cha kamera,
ambako hivi karibuni kupita dawa za kulevya za mabilioni. Waziri
amefanya ziara hiyo siku tatu baada ya kuahidi kuhakikisha inawatia
mbaroni watu wanaojihusisha na usafirisha wa dawa za kulevya kupitia
viwanja vya ndege nchini.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja wa Usalama wa JNIA, Clemence
Jingu, alikiri kuwa Dr. Mwakyembe alifanya ziara hiyo ya kushtukiza
ambapo alioneshwa maeneo pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa
uwanjani hapo wakati wa ukaguzi wa mizigo. Aidha Dr. Mwakyembe
alitembelea eneo ambalo dawa za kulevya zilizokamatwa Afrika Kusini
zilipitia.
Alisema Dr. Mwakyembe aliona hali ya ukaguzi
inavyofanyika ikiwa ni pamoja na mitambo inayotumiwa katika eneo hilo na
kubaini kuwa dawa hizo zilionekana katika mizigo lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa hali inayoonyesha kuwa huenda kuna njama zilizofanywa na
maofisa waliokuwa wanakagua mizigo hiyo.
Taarifa kutoka JNIA
zinaendelea kusema, watendaji wa JNIA walikiri kuwa siku ya tukio eneo
hilo lilikuwa na maofisa Polisi pekee kwa kuwa mbwa wanaotumika kubaini
dawa hizo walicheleweshwa kufika.
Dr. Mwakyembe ameahidi kuwa
“kama sehemu ya wajibu wake wa kulitetea Taifa hili, anajitoa muhanga
kuhakikisha Wizara yake inawatia mbaroni watu wanaojihusisha na
usafirishaji wa madawa ya kulevya, kupitia viwanja vya ndege nchini.”
No comments:
Post a Comment