Dawa za kulevya balaa,
mamia wako jela nje
E MOLA NUSURU KIZAZI HIKI |
MADAWA YA KULEVYA |
China pekee mpaka sasa ina Watanzania 176
wanaotumikia vifungo katika magereza za nchi hiyo, huku asilimia 99
wakiwa wamekamatwa na dawa za kulevya.
Kutokana na kuwapo ongezeko hilo la wafungwa wa
dawa za kulevya, China imekataa ombi la Tanzania la kubadilishana
wafungwa, ikieleza hatua hiyo itachochea watu wengine kujiingiza kwenye
uuzaji wa dawa za kulevya nchini humo.Hatua hiyo imekuja baada ya nchi
hizo mbili kutofautiana katika mfumo wa sheria, ambapo China mtu
anayekamatwa
na dawa hizo hunyongwa hadi kufa wakati Tanzania mtu anayekutwa na dawa hizo anahukumiwa kifungo.
Akizungumza na Mwananchi Jumamosi, Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally
alisema: “Takwimu halisi tulizonazo kutoka China pekee zinaeleza kuwa
Watanzania 176 wanatumikia vifungo na asilimia 99 ni kwa tuhuma za dawa
za kulevya. Kawaida nchi hiyo adhabu yake ni kifo lakini kesi nyingi
bado zipo katika uchunguzi ambao huchukua miaka miwili.”
Hata hivyo alisema kutokana na uhusiano mzuri wa
nchi hizi mbili, kuna uwezekano mkubwa kwa Watanzania hao kufungwa
kifungo cha maisha pamoja na faini.
Aidha, alisema juhudi za Tanzania kuwasiliana na
China kuhusu uwezekano wa kuwa na mikataba ya kubadilishana wafungwa
ziligonga mwamba, baada ya nchi hiyo kukataa ombi hilo kutokana na idadi
kubwa ya wafungwa hao kutuhumiwa na dawa za kulevya.
“China imekataa kuwa na mkataba wa kubadilishana
wafungwa kwani wanahofu kuwa inaweza ikachochea biashara hivyo. Hivyo
kinachofanyika ni kuwatembelea wafungwa hao mara kwa mara na kuhakikisha
wanapata haki zao na kuwasaidia mawasiliano wao na ndugu zao
wanapotumikia vifungo vyao nchini humo.”
Wakati hayo yakibainika, Jumanne wiki hii Tanzania
ilisaini mkataba wa kubadilishana wafungwa na Thailand, mkataba ambao
utawafanya Watanzania waliofungwa nchini humo kuomba kutumikia vifungo
vyao nchini.
Hata hivyo, takwimu zilizotolewa na Tume ya
Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini, zinaeleza kuwa zaidi ya
Watanzania 103 wamekamatwa nchini Brazil kwa tuhuma za kukutwa na dawa
za kulevya, huku 132 wakikamatwa katika nchi nyinginezo.
Hata hivyo, taarifa zaidi kutoka katika tume hiyo
zinadai kuwa hiyo si takwimu halisi ya Watanzania wanaoshikiliwa nje ya
nchi, bali imetokana na nchi hizo kutoa taarifa kuhusu Watanzania hao,
kwani bado idadi kubwa ya Watanzania wanakamatwa lakini taarifa zao
hazijaweza kuifikia tume.
Akizungumza na Mwananchi Jumamosi jana Kamanda wa
Polisi Kikosi Maalumu cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey
Nzowa alisema tatizo la dawa za kulevya linazidi kuwa kubwa kutokana na
ongezeko kubwa la idadi ya wasafirishaji na watumiaji hapa nchini.
nakilo 165 za Cocaine, watu watano wakiwa na kilo tano za dawa aina ya morphine, watu 9539 wakiwa na kilo 279,521 za bangi na watu 1351 wakiwa na kilo 10,318 za mirungi na walifanikiwa kuteketeza ekari 296 za bangi.
“Mwaka 2011 Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya
kilikamata watu 40 wakiwa na kilo 265 za Heroine, watu 30 wakiwa na kilo
128 za Cocaine, watu 39 wakiwa na kilo 17,257 za bangi na watu 150
waliokamatwa na kilo 100 za mirungi pamoja na kuteketezwa kwa ekari 18
za bangi.
Nzowa anautaja mwaka 2012 kuwa ongezeko lilipanda
mpaka kufikia watu 400 waliokamatwa na kilo 260 za Heroine, watu 138
walikamatwa na kilo 151 za Cocaine na wengine 5548 walikamatwa na kilo
48658 za bangi na wengine 847 walikutwa na mirungi yenye uzito wa kilo
2616.
“Katika watu hawa tuliofanikiwa kuwakamata si
kwamba wote wanakutwa na shehena ya dawa hizi, tunaweza kukamata watu 20
wakiwa na gramu 200 tu, lakini tunaweza kukamata watu wachache wakiwa
na shehena,” alisema Nzowa.
Anasema Februali, 2011 walimkamata mtu mmoja
aliyemtaja kwa jina la Shirena akiwa na shehena ya kilo 176 ya dawa za
kulevya ambaye alizipitisha kupitia bandari bubu.
“Bandari bubu hizi walio wengi wanapitisha dawa za
kulevya kuingiza nchini kupitia majahazi na mitumbwi na wengi wao
wanawatumia wavuvi. mfano tulishawahi kukamata kilo 81 za dawa za
kulevya zilizokuwa zikisafirishwa na jahazi. Tulishakamata kilo 211 za
dawa za kulevya huko Mchinga, Lindi zilizokuwa zikisafirishwa kwa
kutumia njia bubu.”
Alisema mwaka 2011 raia wawili wa nje na
Watanzania wawili walikamatwa Mbezi Jogoo wakiwa na kilo 176 za dawa za
kulevya wakijiandaa kuzisafirisha, lakini taarifa ndizo zilizosaidia.
Taarifa zingine zilidai kuwa katika magereza za
Hong Kong kuna Watanzania 200, ambapo 130 kesi zao zimekwishahukumiwa na
wengine 70 kesi bado zinaendelea mahakamani.
Ukubwa wa mtandao ndani na nje ya nchi
Kamanda Nzowa anasema mawakala na matajiri
wanaosambaza dawa za kulevya wapo ndani na nje ya nchi na wanashirikiana
na kubuni mbinu mpya kila uchao.
“Hawa watu wanawasiliana, kwani Tanzania
tunakamata watu wakitoka nje ya nchi wakiingia na dawa za kulevya hapa
nchini, lakini hawa wamepita nchi kadhaa bila kugundulika, hivyo
Watanzania wanavyokamatwa nje ya nchi si kwamba zinatoka kwa uzembe bali
hawa watu wana njia nyingi wanazobuni kila siku,” alisema.
Alisema ushahidi unakuwa mgumu kuwang’amua baadhi yao kwani
hukana na kutoa visingizio kwamba wanakwenda kufuata nywele, nguo au
mazulia nchini Brazil ambako pia kuna idadi kubwa ya Watanzania
wanaoshikiliwa na dawa za kulevya.
“Baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiondoka
hapa nchini kwenda nje ya nchi kuchukua mizigo yao ya kibiashara ambako
pia wanabeba na dawa za kulevya, na hawa walio wengi wanameza kete.
lakini wengi tunashindwa kuwakamata kwa kuwa hatuna vyanzo vya habari,”
alisema Nzowa.
Akitoa mfano aliwataja raia wawili kutoka nchini
Liberia Diaka Brama Kaba na Njane Abubakar Guinea waliokamatwa na kilo
17 na mwingine 14 uwanja wa ndege, wakitokea nchini Trinidad and Tobago
ambao walisafiri kwa ndege wakipitia Brazil, Johannesburg, Afrika Kusini
na kuja Tanzania, lakini taarifa ziliwasaidia kuwakamata.
Nzowa alisema mpaka sasa hakuna mwanasiasa wala
kiongozi wa Serikali anayetuhumiwa kuhusika na mtandao wa dawa za
kulevya, bali kuna baadhi ya wafanyabiashara maarufu wanaochunguzwa
wakiwamo baadhi waliofikishwa mahakamani, lakini wanakosa vidhibiti kwa
kushindwa kuwakamata na chochote kile.
“Changamoto ni kubwa, mpaka sasa tayari Ayoub
Mfaume Kiboko na Shikuba ambaye hupeleka watu wake China na tayari kuna
Watanzania wameshatoa ushahidi huko Hong Kong kumhusu, huyu
tulishamfikisha mahakamani ila pia tulikosa vielelezo na hii ndiyo
changamoto,” alisema.
Aidha, Nzowa alisema ili kujidhatiti katika
kukomesha biashara hiyo wafanyakazi wote wa Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere wakiwamo TAA, Uhamiaji na wengineo washirikiana ili kuweza
kuwabaini wale wote wanaopitisha dawa hizo kupitia kiwanja hicho.
Takwimu za watu waliokamatwa ndani ya nchi ambao ni raia wa
kigeni na Watanzania zinaonyesha ongezeko kubwa kwa mwaka 2012,
ukilinganisha na miaka miwili ya nyuma.
“Mwaka 2010 kitengo kilifanikiwa kukamata watu 496
wakiwa na kilo 191 za Heroin, watu 525 wakiwa
No comments:
Post a Comment