LEMBELI :
VIGOGO SERIKALINI NI MAJANGILINI
|
SILAHA |
Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira imesema vigogo wakubwa
wa serikali wanaongoza kwa kujihusisha na biashara ya pembe za ndovu
ndiyo maana zoezi la kuzuia majangili halifanikiwi kwa miaka mingi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa James Lembeli (MB), alitoa kauli
hiyo ijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya Kamati yake kumaliza kikao
katika ofisi ndogo za Bunge na kusema kuwa wabunge wamepiga kelele kwa
muda mrefu kuhusu tatizo la ujangili wa kuua tembo, lakini serikali
inawapuuza kwa kuwa vigogo wake ndiyo wanaohusika.
Mheshimiwa Lembeli alisema vyombo vya dola navyo watumishi wake
wanahusika kwa kuwa wanaona wakubwa wao ambao ni vigogo wa serikali
wanafanya biashara hiyo haramu ambayo inazidi kuangamiza tembo kila
mwaka.
Lembeli alitanabahisha kuwa Kamati yake mara kadhaa
imekuwa ikishauri namna ya kukabiliana na vitendo vya ujangili wa kuua
tembo, lakini serikali imekuwa haichukui hatua na kwamba baadhi ya
bandari ikiwamo ya Dar es Salaam zinatumika kusafirisha meno ya tembo.
Aliongeza kuwa mwaka 2011, Rais Jakaya Kikwete alitembelea Wizara ya
Maliasili na Utalii na kuwauliza kama wanahitaji awaongezee nguvu ili
kupambana na ujangili, lakini wao mpaka sasa wamekaa kimya hawajasema
kama wameshindwa ili wapatiwe msaada.
Majangili wanatumia
silaha nzito na maboga kwa kuyaweka sumu na tembo anapokula humchukua
dakika 20 kupoteza uhai na hapo majangili hao huchukua meno yao. Meno ya
tembo hutengenezea vitu vya urembo kama pete, bangili, mikufu na vitu
hivyo huvaliwa na watu wakubwa kama wafalme na malkia.
Hivi
karibuni, baadhi ya watumishi katika vyombo vya dola wakiwamo askari
polisi na wanajeshi wamekuwa wakikamatwa na meno ya tembo matukio ambayo
yanaelezwa kuwa ni hatari kwa kuwa wao ndiyo walinzi wa usalama na
maliasili za taifa.
No comments:
Post a Comment