Waislamu watakiwa kuenzi maadili ya dini wakati wote
Chalinze. Wananchi katika Kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo
wameaswa kujiheshimu na kuenzi maadili mema ya kidini kwa miezi yote kila mwaka na siyo wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan pekee.
wameaswa kujiheshimu na kuenzi maadili mema ya kidini kwa miezi yote kila mwaka na siyo wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan pekee.
Pia wameshauriwa kupendana na kushirikiana bila
kujali itikadi za kidini, kabila na siasa ili kupunguza migogoro
inayochochewa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi.
Rai hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kijiji cha
Vigwaza wilayani Bagamoyo, Mohsin Bharwani wakati akitoa sadaka ya
vyakula na mafuta ya kupikia kwa wanakijiji wa vitongoji 12 na waumini
wa misikiti 14 wa kata hiyo. Watu hao walipatiwa kilo 7,000 za mchele,
ngano kilo 250 na mafuta ya kupikia lita 300.
No comments:
Post a Comment