Bosi Necta ateuliwa Rais
Mitihani barani Afrika
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania ( Necta), Dk Joyce Ndalichako, ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Serara Moahi wa Botswana.
JICHO LA AFRICA LAMULIKA ...(TZ) |
“Hii ni heshima ya pekee kwa Baraza la Mitihani
Tanzania, kipindi cha mwaka mmoja nikiwa Rais wa AEAA nitaendeleza
yaliyoanzishwa na mtangulizi wangu, pia kutekeleza ajenda mbalimbali
zitakazoleta manufaa kwa nchi yetu,” alisema Dk Ndalichako. Pia, alisema
atajitahidi kuwa mbunifu na kupanua ushirikiano na nchi nyingine.
, kuhakikisha anawajengea uwezo zaidi wafanyakazi wa mabaraza ya mitihani kwa nchi wanachama.
“Kwa mfano kwetu naona changamoto kubwa ni suala
la standardisation (kusanifisha alama za mitihani), nitajitahidi
kuhakikisha watu wetu wanajengewa uwezo kwenye nyanja hii,” alisema.
Alitumia fursa hiyo kushauri nchi za Afrika
kuhakikisha zinatilia mkazo zaidi kuongeza walimu wa kutosha, walio bora
na vifaa vya kujifunzia. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, Selestine Gesimba, alisema kupata cheo hicho ni heshima kwa
nchi yetu ya Tanzania.
ZIGUA SIMO NA NJERO |
No comments:
Post a Comment