Saturday, 20 April 2013

KIJIJINI KWETU....Mandera , Kwamagome....ya Tanga

ndugu na jamaa -kijijini Mandera
 Matembezi yangu mkoani Tanga nilitembelea kijijini kwangu Mandela na Kwanmagome Handeni Tanga nilikaruibishwa na nduguzangu , jamaa marafiki wote walifurahia ujiu wangu na kukumbushana mengi ya miaka ya nyuma iliyo pita tulitembelea maeneo ya kijijini kwetu , tulisalimiana na ndugu tulikunywa na kula kwa pamoja.....





KIJIJI CHA MANDELA  KIPO WAPI? HUKO MKOANI  TANGA?
Kakweli kijiji cha Mandera kipo Mkoani Tanga Wilaya ya Handeni kijiji cha Mandera na ukitaka kukikifikia itakibidi utoke mjini Handeni na uwe ukielekea njia ya kwenda Korogwe itakuchukia kati ya dakika 30 au 4
kijiji cha mandera
 45 kukifikia kijiji hicho unapotoka Handeni utaelekea stendi ya Chogo ambayo ni stendi ya mabasi ya Handeni utakwenda moja kwa moja hadi ukitane na njia panda mpya ya kutokea Chanika ya Handeni ineyo unganika na ya kwenda Korogwe utakwenda kwa muda wa dakika kadhaa ndipo utakapo iona barabara wa vumbi upande wa kushoto ukiwa ukielekea Korogwe utapinda na kuendelea na njia hiyo ya vumbi kwa muda wa takribani wa dakika 15 niyo ukutane na kijiji hicho cha MANDERA sasa ukienda mbele zaidi utajikuta ukielekea kijiji kingine cha KWAMADULE huko ndiko wazaza wangu waliko tokea.....kijiji hiki kilisifika sana kwa kuwatoa wazee walio tumikia selikari ya awamu ya kwanza wakiwemo walimu askari na wakuu wa idara nyingine nyeti katika nchi hii .....huo mti unao uona ndipo palipokuwa mji wetu wa zamani
kijiji cha kwamagome

...Kijiji cha kwamagome tilipata bahati ya kuku tembelea nako tulipata mapokezi ya kufa mtu tulikula na kunya kwa pamoja na kufurahia ndhari nzuri ya kijijini kwetu kwamagome nikweli " MKUMBUKA KWAO SI MTUMWA"...Nawakaribuisheni kijijini kweti HANDENI......Mjioneee.

No comments:

Post a Comment