CHAKULA CHA
KITAMZANIA
Napenda
kukitambulisha chakula hiki kitamu cha Kitanzania hapa pana ugali, listi nyama,
Dagaa wa kupwaza ….. mchicha ugali mweupe uliopikwa kwa kiasili wa Kitanzania
maandalizi yake ni vyepesi tuu tukianzia kwa uandaaji wa ugali:
UGALI:
Andaa unga mweupe wa kutosha andaa maji
ya moto mekoni (jikoni) baada ya maji kuchemka weka unga kwenye maji yanayo
chemka anza kusonga hadi unga na maji yachanganyike na unga ule ulio uweka
katika maji yale yalio chemka na kukuonyesha mchanganyiko ule umekamilika na
kukuonyesha yakuwa mchanganyiko ule umeiva kwahiyo huo utakuwa ugali umeiva.
MCHICHA:
Andaa mchicha vitunguu, nyanya, Mafuta au karanga tui la nazi tenga
mchicha huo jikoni kwa muda utaona maji yakitoka kwenye mchicha ule na mchicha
ule kuanza kubadilika na kuwa rangi ya kijani na kujitokeza maji chemsha kwa
muda mfupi…..toa mchicha wako jikoni weka sufuria nyingine jikoni weka mafuta,
karanga au tui la nazi. Kama ni kwa mafuta kaanga vitunguu weka chumvi kwa muda
mfupi weka mchicha changanya hadi urudhike mchanganyiko huu upo sawa hapo
itakuwa imeiva…….
DAGAA
WA MCHUZI: Tayarisha dagaa wako wakavu kwa kuwakosha na kuwaondoa
uchafu wakaange kwa muda mfupi na zisikauke sana weka nyanya vitunguu hakikisha
mchanganyiko huo unaiva vizuri hadi kuonyesha mchanganyiko huo umeiva hapo
ndipo utakapokuwa mwisho na mwanzo wa kuliwa….tenga vuzuri chakulahicho cha
kitanzania na anzakula ni chakula kitamu sana hasahasa ukishushia kwa maji ya baridi.
No comments:
Post a Comment