Tuesday, 10 September 2013

Wanaswa na dawa za kulevya Ethiopia




Maporomoko ya Rusumo



Dar es Salaam. Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.
madawa ya kulevya
Bangi
Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo.
Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6bilioni.
Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni).
Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo alithibitisha jana kwamba wanamichezo hao wanashikiliwa nchini humo na Polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.
Wanamichezo hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakamu Kuu ya Ethiopia iliyoko kwenye eneo la Arada, Addis Ababa kujibu tuhuma za kubeba kilo saba za dawa hizo haramu. Mkwanda anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu. Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
Alisema uwezekano wa kesi ya Kaniki na Matumla kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi hizi mbili hazina utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
“Wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10 sasa, sisi tulipigiwa simu na polisi wa hapa Alhamisi iliyopita kujulishwa kwamba kuna Watanzania wawili wameshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na Matumla,” alisema Shelukindo.
“Wao wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na huo mzigo walipewa na mtu mmoja. Lakini Kaniki yeye anajitetea kwamba huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa anajuana vizuri na Mkwanda. “Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu. Walikuwa wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo warudi Sweden kwa njia zao wanazojua wenyewe. Walipofika hapa Mkwanda alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo mingine ilikuwa ya Mkwanda.
“Ndipo hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege wakashikiliwa na Jumatatu ya wiki iliyopita wakapandishwa kwenye Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini hawakupewa nafasi ya kujitetea. Kesi itatajwa tena Jumanne (leo) na Jumatano (kesho) na uchunguzi wa polisi bado unaendelea.”
Wanamichezo hao walidai kwamba walikabidhiwa mizigo hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mombasa walipokuwa wakikabidhiwa pasi za kupandia ndege baada ya kupita sehemu zote za ukaguzi.


“Kilichotokea ni jambo la aibu kwa nchi na hata wachezaji wenyewe wanajuta. Kwa mfano, Kaniki anasema alikuwa aende England kucheza mpira Desemba lakini sisi tukamwambia hatuwezi kumsaidia inabidi akabiliane na kesi iliyoko mbele yake. Mkwanda yeye ametuambia kwamba anaishi Sweden hatuna maelezo yake zaidi,” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa wamewapelekea wanamichezo hao msaada wa mablanketi kwa vile bado wako mahabusu na Ethiopia kwa sasa kuna baridi kali.
Shelukindo alisema wachezaji hao wapo mahabusu kwenye Kituo cha Polisi cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (Federal Police Crime Investigation) na hawana chochote zaidi ya nguo walizokuwa wamevaa.
Watanzania wengine kuachiwa leo
Shelukindo alisema kuna Watanzania wanne wanaotazamiwa kuachia leo baada ya kumaliza vifungo vyao baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.
“Kuna Watanzania wengine walinaswa hapa miaka ya nyuma wao walikuwa wamemeza wakapasuliwa dawa zikatolewa na baadhi yao walifariki. Hata hivyo, wanne ambao wamemaliza vifungo vyao vya miaka minne wanaweza kurudishwa Tanzania,” alisema Shelukindo.

Twiga mdogo

Monday, 9 September 2013

‘Wahamiaji walioolewa ruksa kuishi na wenza’



 
Kilimanjaro   



 OPARESHEN KIMBUNGA

Bukoba. Serikali imesema wahamiaji haramu walioolewa na Watanzania wanaruhusiwa kubaki nchini, hawalazimiki kuvunja ndoa zao ingawa wanatakiwa kupata kibali maalumu kutoka Idara ya Uhamiaji.
Akizungumza mjini hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, alisema wahamiaji haramu walioolewa wanatakiwa kwenda Idara ya Uhamiaji kupata hati hizo.
Rusumo
Kikosi kazi
“Hatupendi kuachanisha familia zilizoishi kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo, wanatakiwa kwenda uhamiaji kuhalalishwa na baadaye ikigundulika hana tatizo anaweza kupewa uraia,” alisema Kanali Massawe.
Pia, alisema kwa mujibu wa sheria, mhusika atapewa kibali alichokiita ‘Independence Pass’
kitakachomwezesha kuendelea kuishi  nchini na kwamba, kinyume chake itakuwa ni kuvunja haki za binadamu.
Hata hivyo, Massawe alibainisha kuwa lazima zoezi la kuondoa wahamiaji haramu lifanyike, kwani walioondoka kwa hiari ni 11,601 na waliokadiriwa kuondoka ni kati ya 52,000 na 53,000, hivyo idadi kubwa bado wanaishi nchini.
Maafisa Uhamiaji
Akizungumzia zoezi la kurudisha wahamiaji haramu lililoanza rasmi Septemba 6, mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma, Mkuu Msaidizi wa Operesheni hiyo, Simon Sirro, alisema tayari wamewakamata  1,851.
Pia, Sirro alisema ng’ombe 1,765, sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na bunduki saba vimekamatwa  na kwamba, wahamiaji  wanaokamatwa wanarudishwa kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia haki za binadamu.

M23 wameahidi kuendeleza mapambano ikiwa leo hawatafikia makubaliano






Wawakilishi wa kundi la upinzani la  M23 wanatazamiwa kukutana na maofisa wa Serikali ya Kinshasa leo  katika mji mku wa Uganda, Kampala kwa lengo la kujadili njia za kumaliza mapigano mashariki mwa Kongo.
WAPIGANAJI WA... UN
KIKUNDI CHA... M23
Rais Kabila alisema juhudi zitafanyika kufanikisha mazungumzo ya Kampala lakini alionya kuwa iwapo mazungumzo hayo hayatafanikiwa jeshi litaendeleza oparesheni dhidi ya waasi.
Juzi Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alifungua mazungumzo ya maelewano ya kitaifa ambayo yanawashirikisha wapinzani na makundi ya kijamii.
Katika ufunguzi wa kikao hicho cha wiki mbili viongozi kadhaa wa upinzani hawakushiriki huku wakimtuhumu Kabila kuwa anapanga kutawala kwa muhula wa tatu mfululizo kinyume cha sheria.

Kabila ambaye muhula wake unamalizika mwaka 2016 alisema mazungumzo hayo yanalenga kujadili sababu za kudhoofika utendaji kazi wa taasisi za kiserikali, pamoja na mapigano Mashariki mwa nchi hiyo ambayo yalianzishwa na wapinzani wa M23miezi 18 iliyopita.
Mazungumzo hayo ya kitaifa ambayo yalipangwa kuanza mwezi Novemba mwaka jana yalianza katika hali ambayo Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya wapin
Mafanikio hayo yalipatikana kutokana na uungaji mkono wa kikosi cha uingiliaji cha Umoja wa Mataifa.
Wito uliotolewa na viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu wa kuitaka Serikali ya Kongo ikae meza moja na  M23 kwa ajili ya kutatua mgogoro wao, ulipokewa kwa mikono mwili na waasi hao, ingawa wametoa angalizo la kurudi tena kwenye uwanja wa mapambano iwapo watachokozwa.
Awali kiongozi wa kundi hilo la  M23, Betrand Bisiimwa, alipongeza uamuzi huo wa kuwataka wakutane na Serikali ya Kongo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wao ambao umedumu kwa muda mrefu.
Bisiimwa akizungumzia uamuzi huo uliofikiwa hivi karibuni katika kikao kilichoketi Uganda, kilichowashirikisha Rais Jakaya Kikwete, Paul Kagame wa Rwanda, Joseph Kabila wa Kongo, Yoweri Museveni wa Kongo na wengine, alisema kikundi chake kilifanya juhudi kama hizo kwa zaidi ya miezi kumi iliyopita, lakini Serikali ya Kongo iliwapuuza, hivyo kusisitiza kwamba wapo tayari kwa mazungumzo au kuendelea na mapigano.
“Naupongeza wito wa viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu kwa sababu wameona umuhimu wa kuyaokoa maisha ya Wakongomani wa hapa mjini Goma, siku zote amani inatafutwa kwa makubaliano ya kukaa meza moja, lakini ukiamua vita hauwezi kushinda,” alisema Bisiimwa.
SIMBA
 

Sunday, 8 September 2013

Wanafunzi 868,030 kuhitimu Darasa la Saba....Tanzania



 
Maporomoko ya maji


Dar es Salaam. Wanafunzi 868,030 wa Darasa la Saba wanatarajiwa

kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Jumatano na Alhamisi wiki hii, ikiwa ni mwanzo wa mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa utakaotekelezwa kwa kuanzia katika mitihani hiyo.
  Taarifa ya Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), inaonyesha kuwa wanafunzi hao wanatoka kwenye shule 15,677 zikiwamo za umma na binafsi.
  Inaeleza taarifa hiyo kuwa, wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani wa lugha ya Kiswahili ni 844,810  kati yao wasichana wakiwa 444,475 na wavulana 400,335.    Kati ya wanafunzi hao, wasioona ni 88 wavulana wakiwa ni 56 na wasichana 32 huku wenye uono hafifu wakiwa 546 na kati yao wavulana ni 263 na wasichana 283.


  Watakaofanya mtihani huo kwa lugha ya  Kiingereza ni 22,535 na kati yao wavulana wakiwa 11,430  na wasichana 11,105.       Wanafunzi wenye uono hafifu kati ya hao ni 51, wavulana wakiwa 21 na wasichana 30.
 Mwaka jana wanafunzi 894,881 kutoka shule 15,363 walifanya mtihani huo, huku wale waliofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili wakiwa 873,837 wavulana walikuwa 415,572 na wasichana 458,265.
  Waliofanya  mtihani huo kwa lugha ya Kiingereza walikuwa 20,457  wavulana wakiwa 10,422 na wasichana 10,035. Wenye uono hafifu walikuwa ni 45 wavulana wakiwa 26 na wasichana 19.
 Msemaji wa Necta, John Nchimbi, alilieleza gazeti hili kuwa tayari mitihani imeshasambazwa huku akionya kuhusu wale watakaojaribu kufanya udanganyifu wa aina yoyote ile.
  “Tunawataka wanafunzi na wadau wote wanaohusika na mtihani huu, wasije wakajihusisha na udanganyifu kwa namna yoyote ile, Necta tupo makini na tumejipanga kwa chochote kitakachotokea,” alisema na kuongeza:


 “Tunaamini kuwa wanafunzi wameandaliwa vya kutosha na wao ni vyema wajiandae zaidi kisaikolojia, yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu tutamchukulia hatua zinazostahili ikiwa ni pamoja na kumfutia matokeo.”
 Wanafunzi hawa wanaanza mtihani wakati ambapo Serikali imeweka lengo la kuinua ufaulu wa mtihani huo kutoka asilimia 31 za mwaka jana mpaka 60 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Maandalizi ya mwisho
Shule mbalimbali za msingi zimeshafungwa tangu Ijumaa iliyopita kati ya wiki moja hadi mbili zikiwaacha wanafunzi wa darasa la saba wakikamilisha hatua za mwisho mwisho kabla ya kufanya mtihani wao.

 Akizungumza jana  kwa simu, Mwalimu Mkuu wa Shule ya High Mount iliyoko Guluka Kwalala Kata ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam, George Mgombozi alisema: “Kwa sasa tunawajenga wanafunzi kisaikolojia baada ya kuwapika vya kutosha.  “Kimsingi, tunachowaambia wanafunzi ni kwamba watambue kuwa wanapofanya mitihani yao waone kama mitihani ya kawaida tu wanayoifanya kila siku,” alisema.
Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mloganzila iliyoko Wilaya  Kisarawe Mkoa wa Pwani, Grace Msele amewataka wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kutumia siku mbili zilizobaki kujiandaa kisaikolojia na  kujiepusha na michezo ya hatari kabla ya kuanza  mitihani yao. Akizungumza kwenye kikao cha wazazi shuleni hapo juzi, Msele alisema kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuwa karibu na watoto wao katika kipindi hiki ili kuwajengea uwezo.

Mtoto wa Kitanzania

Thursday, 5 September 2013

CHEKA KWA RAHA ZAKO

 
 
 
  CHEKA KWA RAHA ZAKO :

JANJA alipita sehemu isiyoruhusiwa katika kambi ya jeshi na akapewa adhabu ya kuhamisha tofali 1,000.

JANJA akajitahidi akabeba tofal 900 na akawa hoi! Na ghafla akakumbuka kuwa Mkuu wa Kambi ni rafiki yake walisoma pamoja, akampigia simu.

JANJA : Mkuu, vijana wako wamenipa adhabu ya       kuhamisha matofali 1000!

MKUU WA KAMBI : Hao wajinga kweli hawajui tunavyofahamiana! Wasikusumbue, mimi ndio mkuu wao. Zirudishe palepale zilipokuwa mwanzo, halafu uje ofisini tuonane.
 
 

Mwanamke ambaye ni raia wa Nigeria....na madawa ya kulevya



Kilima njaro
 Wakati watanzania wakuwa katika mtihani mkubwa wa kupambana na wimbi zito la sintofahami kwa raia wake kujihusisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya ...Raia wa Nigeria nae abambwa katika kiwanja cha ndege cha Tanzania... (JNIA)..............

 Dar es Salaam. Mwanamke ambaye ni raia wa Nigeria, amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akiwa na kete 99 za dawa za kulevya.
Hata hivyo kete hizo hazikujulikana ni za aina gani.
Kukamatwa kwa raia huyo, kumekuja wiki tatu tangu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kutangaza vita dhidi ya watu wanaopitisha dawa za kulevya katika idara na taasisi zilizoko chini ya wizara yake.
Akizungumza na Mwananchi jana, Meneja Usalama wa uwanja huo, Clemence Jingu, alisema mtuhumiwa alikamatwa jana saa 8:00 mchana
Alisema kete hizo alikuwa ameziweka katika makopo ya poda na mafuta.
“Kete hazijajulikana ni za aina gani, kwa sasa tunafanyika utaratibu wa kutambua aina yake,” alisema.
“Kwa sasa hapa JNIA kuna mitambo ya kisasa ya kuweza kuwabaini wanaopitisha dawa hizi, tulimkamata akiwa na kete 99, kati ya hizo kete 30 alikuwa ameweka katika kopo la mafuta ya nywele, kete nyingine alikuwa ameweka katika kopo la poda za watoto,” alisema.
Unga
Alisema kuwa raia huyo wa Nigeria alikuwa akielekea Roma, Italia kupitia Paris, Ufaransa kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
“Baada ya kumhoji ametueleza kuwa dawa hizo alizinunua maeneo ya Magomeni, kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano zaidi,” alisema.
Alisema kuwa binti huyo aliingia nchini Agosti 30mwaka huu, akitokea nchini Nigeria.

Nyani

Museveni awakutanisha Rais Kikwete na Kagame



kilima njaro

Rais wa Uganda

Dar es Salaam. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa dharura wa marais wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais wa Rwanda
Rais wa Tanzania

Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano huo
ambao pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Wakati hali ya usalama

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikidhoofika, katika siku za karibuni, uhusiano wa Tanzania na Rwanda umekuwa wa shaka hasa baada ya Rais Kikwete kuishauri Serikali ya Rwanda kukaa na wapinzani ili kumaliza mzozo uliolikumba eneo la Maziwa Makuu.

Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), zilizofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano wa leo utafanyika kwenye Ukumbi wa Commonwealth Resort, Munyonyo katikati ya Jiji la Kampala.

Kwa mujibu wa taarifa Rais Museveni ameitisha mkutano huo hasa kuzungumzia hatua ya Umoja wa Mataifa kupambana na Kundi la Waasi wa M23.

Mbali na viongozi hao wa Tanzania na Rwanda, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo wanatoka Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan, na Zambia.

Twiga